Sheikh Shaban Issa Bin Simba (78)
(Picha hii ilipigwa 28/7/2014 Wakati wa Swala ya Eid El Fitir, viwanja vya Mnazi Mmoja).
MWILI wa Mufti na Sheikhe Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaban Issa Bin Simba unatarajiwa kusafirishwa kesho mkoani
Shinyanga.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania
(Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Alhad Mussa Salum amesema swala ya marehemu itafanyika katika Msikiti wa Al Farouq Kinondoni jijiji Dar es Salaam asubuhi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
dini na serikali.
Aidha taarifa kutoka kwa Mtoto wa marehemu Suleiman Issa Simba inasema kuwa Mwili wa marehemu utasafirishwa leo na kuzikwa leo hii 16/6/2015 Majengo mkoani Shinyanga majina ya saa 10:00 jioni.
Awali palikuwa na mvutano baina ya familia na BAKWATA juu ya siku ya mazishi lakini familia imesisitiza wosia wa marehemu kuwa asicheleweshwe kuzikwa pindi mauti yakimfika.
Amesema
marehem alikuwa akisumbuliwa na sukari,Shinikizo la Damu (BP) pamoja na
Figo.
Hata
hivyo amesema kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika
Hospitali ya TM Jijini Dar es Salaam na Mauti ya Mufti yamekuta majira ya saa3:45 leo asubuhi.
SALAM ZA RAMBI RAMBI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti
Sheikh Issa Bin Shaaban Simba.
Marehemu Mufti amefariki leo
15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa
na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure).
"Kifo kinaleta huzuni,
hata hivyo Kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea
Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele". Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.
"Nawaombea subra wana familia, ndugu, jamaa, waislamu wote
na wana jamii kwani Mufti alikua kiongozi katika Jamii yetu'” Rais
amesema na kueleza kuwa "Kamwe
mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa Ujumla na hakika sote
tutamkumbuka" ameongeza.
Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka
1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na
Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.
Rais amemuelezea Marehemu Mufti kama
mwalimu katika jamii ambaye alikua na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda
dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka
"Amekua mwalimu imara
na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika uislamu na jamii kwa ujumla, hakika
tutamkumbuka siku zote' Rais Kikwete ameongeza.
Shekhe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa
na uzoefu mkubwa ndani ya BAKWATA na aliwahi kukaimu nafasi ya
mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.
Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi
wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake
pahali pema Peponi, Amina.
0 comments:
Post a Comment