Mahakama
Kuu ya India imemtupa jela miaka mitano Mwigizaji nguli wa Bollywood, Salman
Khan baada ya kukutwa na hatia ya kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi
wengine wanne na kukimbia katika ajali ya barabarani iliyowakumbwa watu hao wasio na
makazi.
Tukio
hilo lilitokea mnamo mwaka 2002 katika mji wa Mumbai na kesi hiyo kudumu kwa
miaka 13 hadi inatolewa hukumu yake.
Khan
katika utetezi wake aliiambia Mahaka kuwa aliyekuwa akiendesha gari hilo
lililowaparamia watu hao ni dereva wake na si yeye lakini Mahakama ilisema Khan
ndie alikuwa akiendesha na alikuwa amelewa.
Wataalam
wa sheria nchini humo bado wanatoa nafasi kwa muigizaji huyo kukata rufaa dhidi
ya hukumu hiyo.
Aidha
taarifa zinasema Mwanasheria wa Khan, tayari amesha wasilisha hati ya rufaa Mahakama
Kuu ya Bombay na huenda ikasikilizwa mapema.
Khan
ni mmoja wa wacheza filamu wakubwa wa Bollywood na ameshiriki katika kucheza
filamu zaidi ya 80 za kihindi.
Miongoni
mwa filamu zake ni pamoja na Dabangg, Ready, Bodyguard, Ek Tha Tiger, Maine
Pyar Kiya na Hum Aap Ke Hain Kaun, na ambazo zimepata mauzo makubwa duniani.
0 comments:
Post a Comment