Nafasi Ya Matangazo

May 06, 2015

 Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu mgogoro wa ardhi katika Kijiji cha Himo na Kiraracha dhidi ya familia ya Sananga inayodai kuporwa ardhi yao na Halmshauri ya Moshi Vijijini.
 Baadhi ya wakazi kutoka katika vijiji vya Himo na Kiraracha waliopiga kambi nyumbani kwa mbunge huyo Sinza jijini Dar es Salaam mpaka hapo watakapopata ufumbuzi wa suala hilo. Kutoka kulia ni Festo Sananga, Yohana Sananga na Mary Amedius.
Baadhi ya wakazi kutoka katika vijiji vya Himo na Kiraracha waliopiga kambi nyumbani kwa mbunge huyo Sinza jijini Dar es Salaam mpaka hapo watakapopata ufumbuzi wa suala hilo. Kutoka kushoto ni Paul Sananga, Dismas Luca Lekule na Denis Amedius Lekule.

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Dk. Augustino Mrema ambaye pia ni mbunge wa Vunjo Mkoa wa Kilimanjoro amemtaka Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kurudisha maeneo ya makazi kwa mahitaji ya wananchi wa Himo Mkoani Kilimanjaro.

Hayo aliyabainisha Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugawaji wa ardhi ambao hauzingatii mahitaji ya jamii ya wananchi hao ikiwepo umilikishaji wa ardhi kwa watu binafsi bila kuzingatia maeneo hitajiwa kwa huduma za jamii zao.

Alisema takriban wananchi 381, wanalalamikia ugawaji huo ambapo kumekuwa na ukiukwaji wa sheria ya ardhi namba 14 ya 1999 na kanuni zake za 2001 ambao unadhibitishwa na barua kumbu; LD/NZ/383/22/DW ya Machi 11, 2013 kutoka kwa kamishna wa ardhi kanda ya kaskazinni ambaye alionekana kufuatilia kwa mwenyekiti wa Serikali za mitaa kuwa ugawaji huo haukuzingatiwa.

"Serikali imetafuta ardhi kwa ajili ya wawekezaji tangu 2006 wakati hata jiwe la msingi hawajaweka hadi sasa, waligawa kienyeji na sasa wanataka kuhalalisha," alisema.

"Ni muhimu kwa wananchi wa Himo kwa sasa na wakati ujao kuwa kuwa na eneo la upanuzi wa shule ya msingi Mieresini, Eneo la soko kwa mahitaji ya sasa na wakati ujao kulingana na idadi ya watu inavyoongezeka, eneo la kujenga mahakama hasa kupunguza kero ya huduma hii kwa mbali,

"Eneo la kujenga chuo cha ufundi cha umma, eneo la kujenga viwanja vya michezo na kujenga afya, maeneo ya biashara na maeneo ya kuabudia pia maeneo ya kuzikia na uwekezaji," alisema Mrema.

Aidha alisema, Aloyce Kimaro ni mmoja wa matajiri waliomilikishwa eneo la ekari 11.7, kwa ujenzi wa kituo cha redio na Edward Shayo ambaye anamiliki asilimia 75 ya ardhi ya Himo.

"Hii Serikali ni ya kipuuzi, nipo tayari kung'oka ubunge lakini nikitetea wananchi wangu, siwaogopi nitawataja matajiri wanaomiliki ardhi tangu 2006 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha redio lakini hadi leo hakuna hata jiwe la msingi, kwani kituo hicho ni hewa," alisema Mrema.

Aliongeza kuwa tajiri mwingine ambaye ni mkazi wa Arusha mwenye jina la Minja amemilikishwa ekari 7, kwa matumizi ya kujenga kituo cha watoto wa mitaani, na kusema kuwa kituo hicho ni hewa kwani hakuna dalili zozote za kujengwa kwa kituo hicho.

"Utashaangaa kuona shule ya msingi inawatoto 400 lakini imemilikishwa ekari 5 tu ambazo hazitoshelezi. Pia ugawaji huo umemilikisha ekari 1.7 kwa ajili ya super maket ya halmashauri lakini maeneo mengine kumilikishwa marehemu kama Mariam Mfinanga, mita za mraba 9277, kwa ajili ya makazi ambaye alifariki miaka mingi kabla ya ugawaji huo.

Alisisitiza kuwa Lukuvi ndiye mwenye dhamana kisheria kwani amelisema sana kelele bungeni bila mafanikio yoyote, hivyo ayatafutie ufumbuzi mapema ili ugawaji urudiwe ili kunusuru wananchi wa himo kuchukua hatua ya uvunjifu wa amani kwa kudai maeneo hayo wenyewe.

Kwaupanda wake Paul Paul ambaye ni mtoto wa marehemu Paul Sananga mkazi wa Kilimanjaro wanaidai serikali kiwanja cha nusu ekari 4 kwa kubadilishana kiwanja cha ekari 2 kwa ujenzi wa shule kwa miaka 14 sasa bila kupewa eneo lingine la fidia amesema hadi sasa hawanamahali pa kuishi na wanamtaka waziri Lukuvi awasaidie kupata eneo lao. 
(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)
Posted by MROKI On Wednesday, May 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo