Mkurugenzi
mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya
mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya Crdb unatarajia
kufanyika kesho jijini Arusha.
Mkurugenzi
mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei,kushoto ni Naibu Mkurugenzi
mtendaji huduma mtambuka benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka,kulia ni Naibu
Mkurugenzi mtendaji uendeshaji na Huduma kwa wateja CRDB Bw.Saugata
Bandyopadhyay
Baadhi ya sehemu ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha
Godwin Semunyo Meneja mahusiano Benki ya CRDB
Bi.Tully
Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa
wateja akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi
ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB
Kulia
ni Katibu wa bodi ya CRDB John Baptist Rugambo,katikati ni Mkurugenzi
wa Fedha Frederick Nshekanabo,Kushoto Tully Esther Mwambapa ambaye ni
Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa wateja
Mwandishi kutoka TV1 Arusha Jane Edward akijaribu kuchukua taswira katika mkutano huo
Kulia
ni Ena Mwangama Meneja kitengo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu
na Edwin Nchimbi Afisa masoko wakifatilia mkutano huo
Kulia ni Meneja Usajili wa Hisa kuotaka Benki ya CRDB Emmanuel Ng'ui na Dorice Ngikari kutoka ofisi ya Katibu wakifatilia jambo
Mwandishi
wa habari kutoka Mwananchi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Arusha Media
Mussa Juma akiuliza swali kwa Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb
Dr,Charles Kimei
*******
Na Pamela Mollel-Arusha
Kufuatia
anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola wafanyabiashara nchini
wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara
zao ndani na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo
wanalalamikia anguko hilo.
Ambapo
hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali
inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na
wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya
nchi.
Hayo yameelezwa jana
na Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Crdb Dr,Charles Kimei wakati akiongea na
waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini
wa wanahisa wa Benki ya Crdb unatarajia kufanyika kesho jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha Kimataifa AICC.
Hata
hivyo alisema kuwa hivi sasa Banki hiyo imeweza kupata faida ya
shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa
ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida hiyo itawasaidia kuweza
kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya
wanachama hao.
Ambapo
mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu
ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
Dr,Kimei
aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo mkuu
ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na kuongeza
mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza kukabiliana na
wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama wa pesa za
wateja wao.
Aidha
Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza
zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili
kuboresha huduma hizo na kukuza rasilimali za banki hiyo.
Dr,Kimei
aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya Burundi
na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi wanapotoka
na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
Banki
hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na
wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili
kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.
0 comments:
Post a Comment