Ni
ukweli usiopingika kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu!!
Hivi
karibuni kumekua na mfululizo wa makundi mbalimbali ya watu kufurika nyumbani
kwa mwanasiasa hodari,Mh.Edward Ngoyai Lowassa kumshawishi agombee nafasi ya
urais 2015. Hili ni jambo jema sana,pia ni kitu ambacho hakijawahi kutokea
katika historia ya Tanzania.
Sasa nijikite kidogo katika kauli za baadhi ya watu ikiwemo katibu itikadi chama cha mapindizi,ndg Nape Nauye,..wakidai kuwa vitendo hivyo sio vizuri hata kidogo na vinaweza muondolea shujaa huyu (Edo) kugombea nafasi ya urais.
Binafsi nalichukulia kama binafsi kauli zisizo na mashiko na ni kauli za
kupuuzwa na kutupiliwa mbali na watanzania kwani zina lengo la kukosesha
Tanzania kiongozi bora atakayeleta maendeleo kwa watu wa viwango mbalimbali.
Edward Lowassa haandai wala hafikirii kuandaa watu waje kumshawishi kugombea urais, ni mtu aliyefanya mambo makubwa katika nchi hii kwa nyazfa mbalimbali alizowahi kuzishika, hivyo watanzania wanamuhitaji sana kiongozi huyu aridhi mikoba ya Mh.J,M Kikwete ili atende makuu katika ubora wake.
Cha ajabu kabisa Edward Lowassa ni mbunge aliyetekeleza ahadi zake kwa dhati kabisa jimboni kwake monduli na kumfanya mbunge wa nafasi ya juu kabisa kutumikia wananchi katika ukamilifu wake,..amaa kweli lowassa ni jembe.
Ningependa kuwaambia watanzania wasikatishwe tamaa na kauli za wakina Nape ambao wanatafuta kila mbinu kuwavuta moyo watanzania juu ya chaguo lao pekee......na pia watambue ya kuwa zama zile za kuchaguliwa mke na wazazi wako UMEPITWA na wakati, hivyo ni wakati wa kila mtu kwa mtizamo na chambuzi zake kumchagua ampendaye, kwasababu hiyo ifahamike kuwa Nape hana hati miliki ya Ccm, kwani Ccm sio nyumba wala gari lake bali Ccm ni mali ya wananchi wote, hivyo ieleweke hivyo na sio vinginevyo.
Labda ungejiuliza swali,..kwanini baadhi ya makada hawa wanamfuatilia sana Mh.lowassa na kumtungia umbea kuliko mtu yeyote yule? Jibu ni rahisi sana, wanamuhitaji mtu asiye na maamuzi mapana kwa taifa, na ambaye atawawajibisha wazembe bila kujali nani na katoka chama gani......sasa basi watanzania wa leo sio wapuuzi kiasi hicho.Edo ndiye chaguo la watu..
Na labda kwa taarifa yao tu no kwamba makundi mengi zaidi yatatua kwa Edo kuzidi kumshawishi jemedari huyu.
Wavimbe wapasuke lakini ndivyo wanachi walivyoamua. Imani yangu...''kuzuia nguvu ya wananchi kumshawishi Edward Lowassa, kuzuia umaarufu wake, kuzuia utendaji wake, kuzuia imani yake kwa watu wote,...Ni sawa na kuufukuza upepo''
Hivyo basi nimuombe Mh Edward Lowassa kutojibu hoja za kichawi hizi zinazozushwa na watu tusiosita kuwaita wachawi.
0 comments:
Post a Comment