TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) leo kifanya semina ya nusu siku kwa waandishi wa habari mbalimbali waliopo Bungeni mjini Dodoma kuripoti matukio Bungeni.
Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo wanahabari juu ya uelewa wa sheria nzuri za habari na upatikanaji wa taarifa kwa waandishi wa habari.
Mmoja
wa Wawezeshaji kutoka Shule ya Mawasiliano ya Umma na Uandishi wa
Habari (SJMC), Dk Ayub Rioba akiwasilisha mada yake hii leo juu ya
umuhimu wa sheria nzuri na endelevu za vyombo vya habari Tanzania.
Semina hii ya nusu siku inafanyika katika moja ya kumbi za mikutano
Dodoma Hotel mjini Dodoma.
Meza Kuu kutoka kushoto ni Mwalimu wa Sheria na Mtoa mada ya umuhumi wa Sheria ya kupata Taarifa, James Jesse kutoka Shule ya Sheria, Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Dk. Ayub Rioba kutoka SJMC ambaye pia alitoa mada.
Mwezeshaji
mwezeshaji katika semina hii, James Jesse kutoka Shule ya Shjeria ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishusha nondo zake juu ya umuhimu wa sheria ya haki ya kupata taarifa Tanzania.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza mada katika semina hiyo iliyoandaliwa na MISATAN na kufanyika mjini Dodoma leo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza
mada katika semina hiyo iliyoandaliwa na MISATAN na kufanyika mjini
Dodoma leo.
Deus Kibamba (kulia) kutoka Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB) nae alihudhuria na kutoa uelewa wake juu ya sheria hizo ambazo l;icha ya kuwa zinaenda kujadiliwa Bungeni lakini wadau hawajaziona.
Waandishi
wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mafunzo hayo
ambayo ni chachu kufuatia muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari
unaotaraji kuwasilishwa Bungeni wiki Machi 31 mwaka huu mjini Dodoma.
Dk Ayub Rioba akifuatilia hoja za waandishi.
0 comments:
Post a Comment