Hii ni moja ya kipande cha sabuni kilichotumika
kufungaswa na kufanikiwa kumwibia mpita njia shilingi 100,000 alipokuwa
katika harakati za kutafuta simu kwenye mtaa wa Uhuru Dar es Salaam.
Pia hiyo ni aina ya simu mojawapo watumiayo matapeli hao kuibia wapita
njia.
Vijana ambao huzurula maeneo ya Kariakoo bila shughuli maalum wamekuwa wakihusishwa na utapeli kwa kutumia vipande vya sabuni wakikimbia
baada ya kunaswa na kamera ya bloger wetu wakiwa katika jitihada za
kumwibia mmoja wapita njia katika mtaa wa Uhuru Dar es Salaam leo
asubuhi.
Kwa Mujibu wa shuhuda vijana hao huwa kundi na baadhi uangalia
mwenzao akitekeleza uhalifu wakati wao wakihakikisha wanampa ishara ya
kufuatiliwa na kutoa ishara waonapo mazingira ya mchakato kushindikana
ama hali kuwa tete kwa mwenzao iwapo mnunuzi wa simu atakuwa ameshtukia
njama zao mbovu za kutaka kutenda uhalifu.
Mmoja wa wakazi wa Dar es
Salaam alikumbwa na mkasa wa kuibiwa shilingi laki moja alivutiwa na
mhalifu mmoja kwa kumwonesha simu yenye gharama ya sh 200,000 huku
akimsihi anunue kwa sh 100,000.
Alipokubali kununua simu hiyo,
walimbadilishia wakati akitoa hela na alipoikabidhi na kwenda hatua
chache aligundua kuwa amepewa kipande cha sabuni kwenye bahasha wakati
mhalifu huyo na wenzake wameshatokomea asiko kujua.
Jambo la
kusikitisha ni kwamba askari polisi wameshapokea malamiko ya mikasa kama
hiyo lakini hakuna jitihada za makusudi zilizochukuliwa kuwanasa na
kuwatia hatiani wahalifu hao.
Tahadhari inatolewa kwa wananchi kutonunua
bidha kama hizo mkononi kwa watu hasa katika mazingira ya ushawishi
mkubwa na kufanya manunuzi kwenye maduka yenye kutoa risiti kwa bidhaa
walizonunua.
Mmoja wa wahalifu wa wizi wa simu za mikononi akiwa
katika harakati zake za kutimiza adhma yake katika mtaa wa Uhuru jijini
Dar leo.
Hii ni moja ya kipande cha sabuni kilichotumika
kufungaswa na kufanikiwa kumwibia mpita njia shilingi 100,000 alipokuwa
katika harakati za kutafuta simu kwenye mtaa wa Uhuru Dar es Salaam.
Mfano wa mojawapo ya vipande vya sabuni vitumiwavyo
na wahalifu wa wizi wa simu za mikononi kufanyia utapeli. (Imeandaliwa
na Robert Okanda Blogspot)
0 comments:
Post a Comment