MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili
vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa
wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata
janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo
Mtoto huyo aliungua vibaya.
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo
Baadhi ya waandishi wa habari
wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo
MTOTO Adolotea Njavike(1.4)
anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa
upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya
Moto akiwa na mama yake Mzazi.
Akizungumza kwa masikitiko
Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga
Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto
katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo
aliungua vibaya.
Anasema tukio hilo lilitokea
Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya
mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na
kufurahi na wenzake.
Anasema tangu kipindi hicho
alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada
ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo
Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.
Ameongeza kuwa baada ya muda
wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia
mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na
kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar
Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.
Aidha kutokana na kuambiwa
hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka
Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi
DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.
Amesema anahitaji zaidi ya
shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na
huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri
matibabu ya Mwanaye.
Mtu yeyote mwenye kuguswa na
tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya
Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani
kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.
Na Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment