Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa akisalimiana na waombolezaji mara baada ya kuwasili katika kata ya Nzihi Kidamali ambako walienda kushiriki katika mazishi ya vijana watatu wa kijiji hicho waliofariki kwa ajali jana mkoani Iringa, marehemu hao ni Nyakile Luvanda Dereva, Sabasaba Kunzula Kuli, Ansikali Chengula Kuli waliokuwa wakifanya kazi katika kiwanda cha Maji Afrika yanayotengenezwa Kidamali mkoani humo, Katika Mazishi hayo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchema ametoa shilingi milioni moja kama rambirambi kutoka Chama cha Mapinduzi huku akimshauri mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM ndugu Godfrey Mgimwa kuchukua jukumu la kulipia karo za watoto wa familia za marehemu endapo atashinda kiti hicho na kuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa wakiwasili katika kijiji cha Kidamali wakati walipoenda kushiriki mazishi ya wananchi watatu wa kijiji hicho waliofariki kwa ajali jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba akizungumza na wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kidamali.
Majeneza ya miili ya vijana waliofariki kwa ajali katika kijiji cha Kidamali mkoani Iringa yakiwasili katika eneo la makaburi mahali ambapo mazishi yamefanyika.
Majeneza ya miili ya vijana waliofariki kwa ajali katika kijiji cha Kidamali mkoani Iringa yakiwasili katika eneo la makaburi mahali ambapo mazishi yamefanyika.
Majeneza ya miili ya vijana waliofariki kwa ajali katika kijiji cha Kidamali mkoani Iringa yakiwasili katika eneo la makaburi mahali ambapo mazishi yamefanyika.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba akishiriki mazishi hayo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba na mgombea ubunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa wakishiriki mazishi hayo.
Umati wa waombolezaji ukiwa makaburiki ukishiriki katika mazishi hayo.
Mazishi ya miili hiyo yakiendelea.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba na mgombea ubunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa wakiondoka mara baada ya mazishi hayo
Kiongozi wa Chama cha Chadema akizungumza katika mazishi hayo ambapo Chama hicho kimetoa ubani wa shilingi elfu hamsini.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba akizunguza katika mazishi hayo ambapo Chama cha Mapinduzi kilitoa ubani wa shilingi milioni moja taslimu kulia ni mgombea ubunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa
Hili ndilo gari lililosababisha vifo vya vijana hao.
0 comments:
Post a Comment