Nafasi Ya Matangazo

August 26, 2026

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimependekeza jina la mwanachama wake Ndg. Deogratius John Ndejembi kua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Akitangaza uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya CCM iliyokugana leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro amesema hivi sasa zonasubiriwa taratibu za kikatiba ili kukamilisha mchakato huo.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Makamu wa Rais aliyepo madarakani Balizi Dkt.Emmanuel Nchimbi kumwandikia barua Rais ya kutaka kujiuzulu na Rais Samia Suluhu Hassan siku hiyo hiyo ya Agosti 25, 2026 kuridhia barua hiyo.

Ndejembi (43) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoni Dodoma na Waziri wa Nishati atalazimika kuachia nafasi hizo na kushika wadhifa wake mpya wa Makamu wa Rais pindi Bunge likimuidhinisha. 

Ni msomi wa Shahada ya International Relations katika Chuo Kikuu cha Lincoln cha Nchini Uingereza.

Ndejembi alianza elimu ya msingi  Cannon Andrea kuanzia mwaka 1988-1995, kisha akasoma sekondari ya Kigurunyembe mkoani Morogoro mwaka 1996-1998 na Merton College 2002-2004.

Deo Ndejembi ni miongoni mwa wanasiasa ambao wamepanda hatua kwa hatua katika uongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ndejembi alianza kujijenga kisiasa kupitia UVCCM, kabla ya kuingia kwenye nafasi za uongozi wa Serikali.

Kada huyo wa Chama cha Mapinduzi nyota yake ilianza kushamiri mwaka 2016, alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma na Rais Dkt John Magufuli.

Baadae alijitosa kuwania Ubunge 2020 na kushika nafasi mbalimbali ikiwa na Unaibu Waziri Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala Bora).

Julai 2024, Rais Samia alimteua Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na baadae Waziri wa Nishati
Aidha, katika hatua nyingine Chama cha Mapinduzi kimetangaza kumvua uanachama Ndugu. Dkt Emmanuel Nchimbi aliyekua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania.






Posted by MROKI On Wednesday, August 26, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo