Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza
na Wananchi wa Mbuyuni, Moshi Mjini, waliojitokeza kumlaki akiwa katika ziara
binafsi mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 01 Septemba 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasalimu Wananchi wa Mbuyuni,
Wilayani Moshi waliokusanyika kumlaki akiwa katika ziara binafsi mkoani
Kilimanjaro leo tarehe 01 Septemba 2026.
Akiwasalimu wananchi hao,
Makamu wa Rais amewasihi kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na yeye binafsi ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Amesema kwa imani ya maombi ataweza
kumsaidia kwa hekima na utii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais amesema
ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu, umakini na kujituma,
akisisitiza utayari wake wa kushirikiana na viongozi pamoja na wananchi.
Akizungumza kwa msisitizo, Makamu
wa Rais amesema: “Hatawazingua Wana wala hatamzingua Mama,” kauli ambayo
aliitoa pia mkoani Dodoma, kwa wananchi wa Chamwino, mara baada ya kuapishwa.
Awali, Makamu wa Rais aliwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo alipokelewa na
viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa Dini na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, leo tarehe 01 Septemba 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, leo tarehe 01 Septemba 2026.
0 comments:
Post a Comment