MALINZI AUNDA
KAMATI YA MIAKA 50 FIFA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya
watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
TFF
ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo
itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.
Kamati
hiyo itaongozwa na Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel
Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).
Wajumbe
ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela,
Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi
karibuni.
Kamati
itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya
Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.
KILA LA KHERI
YANGA MECHI YA LIGI YA MABINGWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi
yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly
kutoka Misri.
Mechi
hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
Maandalizi
ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na
waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo
inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.
Milango
yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani
(Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo
cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari
maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile
washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au
vifaa vyovyote vya chuma.
MAREKEBISHO YA
MECHI VPL, FDL
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa mechi
mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na moja ya Ligi Daraja la Kwanza (VPL).
Mechi
namba 143 kati ya Tanzania Prisons na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu
sasa imesogezwa kwa siku moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile Machi 8 mwaka
huu Mbeya City itautumia uwanja huo kwa mechi nyingine ya VPL.
Nayo
Mgambo Shooting iliyokuwa icheze na Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga sasa imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka huu kwa vile Kituo
cha Tanga kitakuwa na mechi mbili.
Kwa
upande wa FDL, mechi ya Mkamba Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa Machi 3
mwaka huu badala ya Machi 9 mwaka huu mjini Ifakara. Mechi hiyo imerudishwa
nyuma ili kuipunguzia gharama Kimondo SC kwani Machi 1 mwaka huu itacheza na
Burkina Faso mjini Morogoro.
0 comments:
Post a Comment