Na
Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya CXC ya jijini Dar es Salaam, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na
waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitosa kupiga tafu Mkutano Mkuu wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika kesho.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema NSSF imetoa udhamini
wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja ametoa Sh milioni moja kwa
ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
“Tunashukuru
Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam, waandaaji
wa Tamasha la Pasaka kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF
wametusaidia kwa kiasi fulani mkutano wetu.
“Bajeti
yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama wa Dar es
Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine wanatoka Morogoro,
Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na kuongeza kuwa wanatarajia wanachama
150 washiriki mkutano huo.
Alisema
mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba wanachama
kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari kwa mkutano huo wa
aina yake.
0 comments:
Post a Comment