Nafasi Ya Matangazo

July 11, 2013

Wasanii wanao unda kundi la ZEETOWN SOJAZ King Pozza (kulia) na Kira Kirami wakiwa katika pozi.
 
WASANII wawili wanao unda kundi la mzijki wa kizazi kipya la Hiphop linalojulikana kama Zee town Sojaz  kutoka visiwani Zanzibar wameachia kibao chao cha kwanza kinachokwenda kwa jina la Chinjachinja.
Wasanii hao Joseph Mwingira 'King Pozza na Omari Ali 'Kira Kirami wameuambia mtandao huu kuwa wimbo huo wameufanyia kazi visiwani humo katika studio ya Jupitor chjini ya mwaandaji Aloneym.
Vijana hao ambao wamesema wamepania vikali kushika anga za Hip Hop visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wapo mbioni kupakua albam ya nyimbo zao kadhaa ila kwa sasa wanaupa nafasi wimbo wao huo kufanya kazi kwanza.
 "Tuna mapango wa kutoa albam ila si hivi sasa tunaupa nafasi wimbo wetu huu wa chinjachinja kufanya vyema sokoni ndipo tutoe albam", alisema Mwingira.
Posted by MROKI On Thursday, July 11, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo