Kiongozi wa kikundi cha Basesilia Bujora, akionyesha
umahiri wake wa kucheza na nyoka katika siku ya mwisho wa tamasha hilo ambapo
kikundi chake kiliibuka washindi wa siku hiyo, Tamasha hilo lililodumu kwa
takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti
Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
Wasukuma kucheza na nyoka ni asili yao na hapa ni moja ya burudabni za nyoka zikiendelea.
Umati wa wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia kwa
makini ngoma za jadi kutoka kabila la wasukuma ‘Bulabo’ katika kiwanja cha
Kisesa. Tamasha hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya
wakazi wa jiji la Mwanza lilidhaminiwa
na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
Kwa shangwe
kubwa maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Magu jijini Mwanza wamekuwa wakishuhudia
burudani ya ngoma za asili za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambalo limemalizika
siku ya Jumapili jioni katika uwanja wa Kisesa jijini Mwanza. Katika sherehe
hizo za kiutamaduni vikundi ishirini na nane kutoka makabila ya wasukuma vilishiriki na kuzifanya sherehe hizo zivutie
zaidi. Kampuni ya bia ya Serengeti imeahidi kuendelea kudhamini tamasha la
ngoma za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambazo ni maalum kwa ajili ya kusheherekea
sikukuu za mavuno kila mwaka.
``Tunayofuraha
kubwa kwa mara nyingine tena kuona tumeweza kuungana na wenzetu wa kabila la wasukuma
katika kipindi cha wiki moja sasa na kusherehekea furaha yao baada ya mavuno
huku wakiendelea kuzienzi tamaduni zao. Ni kwa mara ya nane sasa tumekuwa
tukidhamini sherehe hizi za bulabo na tunaahidi kuendelea kudhamini kwani
sherehe hizi zina mchango mkubwa kwa wasukuma na taifa kwa ujumla”. Alisema
jaji Mark Bomani mwenyekiti wa kampuni ya bia ya serengeti.
Kampuni ya bia
ya Serengeti imekuwa ikidhamini tamasha hilo kwa takribani mwaka wa nane
sasa,ambapo waandaaji wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwezesha na kufanikisha
tamasha hilo, ”Napenda kutoa shukrani zetu kwa kampuni ya bia ya Serengeti ambayo
imekuwa mdhamini wetu kwa muda mrefu sasa inafika miaka minane, tumekuwa nao
bega kwa bega na hasa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Mheshimiwa Mark Bomani
ambae pia ni mlezi wetu hapa Bujora” alisema Padri Mhoja, muandaaji wa tamasha
hilo.
Naye mgeni
rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa
Jacquieline Liana, ameipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamini
tamasha hilo na kuomba wadau wengine kujitokeza kudhamini kama wenzao wa kampuni
ya bia ya Serengeti wanavyofanya, pia aliwaasa vijana kuacha tabia za kunywa
pombe wakati wa kazi na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waje
kusheherekea sherehe hizi za Bulabo mwakani.
Katika sherehe hizo za Bulabo vikundi
vilivyoshiriki vilishindana kwa mtindo wa mtoano ambapo vikundi viwili vikiwa
katika pande mbili tofauti za uwanja vikitenganishwa na bendera nyekundu, huku
majaji wakiangalia ni kundi lipi lenye umati mkubwa hivyo ni kuashiria kuwa
mwenye watu wengi zaidi ndiye mwenye mvuto zaidi na hapo kutangazwa mshindi.
Kigezo kingine kichokuwa kikiwafanya washiriki waongeze jitihada katika kucheza
na kujikuta wakiwapa raha zaidi watazamaji ni kile cha kundi linaloshindwa
kutakiwa kutoa elfu thelathini katika laki mbili ambazo zilikuwa zikitolewa kwa
kila kundi na kumpa mshindi.
Washindi katika
ngoma hizo zilizodumu kwa takribani wiki moja ni Nghomi Lukala, Kanigini
Hindiya, Kibola Shitungulu, Bagehu Lukala, Mayokagose, Kinasa Ncheye,
Nyamuitabungagwa Mnkoti, Mabeshi Lukwaja, Nyeyewaza, Shigulu Dema, Bulolo
Shokolo, Seleleko na Basesilia Bujora aliyemalizia siku ya Jumapili baada ya
mpinzani wake kuingia mitini.
0 comments:
Post a Comment