Nafasi Ya Matangazo

June 25, 2026

IMG_6244.JPG
Benki ya NMB imetangaza udhamini wa Sh milioni 150 kufanikisha msimu wa nane wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi—CDF Cup 2026—yatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 6 hadi 17.

Mashindano hayo yatahusisha michezo 13 na timu kutoka Kamandi ya Makao Makuu ya JWTZ, Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Kamandi ya Jeshi la Akiba na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa.

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, alisema udhamini huo unaendeleza ushirikiano wa benki hiyo na majeshi katika kukuza michezo, kuimarisha ushindani na kujenga umoja, afya thabiti na mshikamano miongoni mwa washiriki.

Mashindano yatafunguliwa Julai 6 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, huku yakitarajiwa kutoa jukwaa la kukuza vipaji, kuimarisha utimamu wa mwili na afya ya akili pamoja na kujenga mahusiano mema kwa washiriki.

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro (kushoto), akikabidhi hundi mfano ya udhamini wa Sh milioni 150 kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya CDF Cup 2026, Brigedia Jenerali Saidi Hamis Saidi (katikati), jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Julai 6 hadi 17, yakishirikisha timu za kijeshi katika michezo 13.
IMG_6259.JPG
IMG_6246.JPG

IMG_6247.JPG

IMG_6248.JPG

IMG_6250.JPG

IMG_6251.JPG

IMG_6253.JPG

IMG_6254.JPG

IMG_6255.JPG

IMG_6257.JPG

IMG_6258.JPG

IMG_6245.JPG
Posted by MROKI On Thursday, June 25, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo