Katibu
Mkuu wa Zamani Ofisi ya Rais Ikulu,Mzee Timothy Apiyo (pichani),
amefariki dunia katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini
alikokuwa amelazwa.
Marehemu
Mzee Apiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Ikulu kwa Kipindi kirefu mpaka
alipostaafu na kuhamia Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Anatajwa kuwa ni
mmoja wa viongozi waandamizi waliokuwa hawana masihara kazini, kiasi
hata viongozi serikalini walikuwa wakimheshimu sana.
Mipango
ya kuusafirisha mwili wa marehemu Mzee Apiyo inaendelea nasi
tutawafahamisha kila hatua kwa kadri tutavyopata ripoti hizo.
Timothy
Apiyo, alizaliwa katika wilaya ya Rorya, Tarafa ya Suba, mkoa wa Mara.
Alipata elimu ya msingi na sekondari akiwa hapo na mwaka 1959 alijiunga
na Chuo Kikuu cha East Afrika na kuchukua digrii ya kilimo.
Baada
ya kuhitimu aliingia serikalini wakati huo Tanzania ikiitwa Tanganyika,
na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Mwaka
1959 alihitumu Makerere na kupangiwa kufanya kazi katika Chuo cha
Kilimo cha Ukiliguru.
Mwaka
1960 alihamishiwa wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kuwa Bwana Shamba wa
Wilaya na mwishoni mwa mwaka huo akahamishwa tena kwenda Wilaya ya
Ifakara mkoani Morogoro ambako alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Ilonga.
Alikaa
Ilonga hadi Agosti 1962 ambapo alipata ufadhili wa kwenda kusoma
Marekani katika Chuo Kikuu cha West Virginia ambako alichukuwa digrii ya
pili ya Sayansi ya Kilimo na kutunukiwa cheti mwaka 1963.
Baada
ya kurejea nchini, mwaka 1964 alipangiwa kufanya kazi Wizara ya Kilimo
na baadaye akapelekwa Shinyanga kuwa Ofisa Kilimo wa Mkoa. Desemba 1965
alihamishiwa mkoa wa West Lake (Sasa Bukoba). Na mwakan 1967
akarudishwa wizarani nikiwa Afisa Mipango Mwandamizi.
Mwaka
1968 akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango Kilimo katika Wizara ya
Kilimo na mwaka uliofuata 1969, akawa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Nyumba, Ardhi na Maendeleo Mijini. Novemba 1969 alirudishwa tena Wizara
ya Kilimo kuwa Katibu Mkuu na Aprili 1972 akapata uhamisho kwenda kuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda.
Aprili 1974 Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Julai 1986 alistaafu kazi.
0 comments:
Post a Comment