WASANII wa filamu
nchini wameshauriwa kuwasilisha miswada ya filamu kwa Bodi ya Filamu ilkaguliwe
na kupewa kibali kama unafaa,umefata sheria na haujakiuka maadili ya sheria ya
Filamu na Michezo ya kuigiza pamoja na kanuni zake.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo wakati
wa kikao na mtengenezaji wa filamu Aunt Ezekiel kuhusiana na kazi yake mpya
ijulikanayo kama Scola.
Katibu huyo amefafanua
kuwa kuna umuhimu wa wasanii kufata sheria
na taratibu za filamu kabla ya kuanza kutengeneza na kuzitoa filamu zao
ambapo sheria inawataka kuwasilisha miswada
(script) Bodi ya filamu ili ukaguliwe na kupewa idhini yakuendelea na kazi
hiyo.
“Wasanii mnatakiwa
kuzingatia sheria na kuwasilisha script ili zikaguliwe na kupata ruhusa kwa
mujibu na taratibu za sheria kabla ya kuanza kutengeneza filamu kwa sababu sheria
Na 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na kanuni zake zinataka
wasanii kutotoa au kutengeneza filamu kabla ya kupeleka mswada(script ) kwa Bodi.
Aidha Katibu huyo
amefafanua kuwa wasanii wanapotengeneza picha kupitia script ambazo
hazijakaguliwa kuna uwezekano mkubwa wakuwepo sehemu ambazo zinakiuka maadili
ya mtanzania,ikiwepo uvaaji wa mavazi mafupi yaliyopitiliza kwa waigizaji
wanawake,lugha mbaya na baadhi ya vitendo vingine visivyofaa kuoneshwa kwa
umma.
Bi Fissoo amesema kuwa Bodi
imepewa mamlaka kwa mujibu wa Shetia kuzuia filamu hizo ambazo hazijakaguliwa
,na kama msanii hajafuata sheria atapata hasara kutokana na gharama ambazo
atakuwa ametumia na endapo filamu hiyo itafutwa, jambo a,balo Bodi
isingelipenda liwakute wadau wake.
Kwa upande wake Msanii
wa Filamu za Kiswahili Aunty Ezekiel ameomba radhi kwa kutoleta script yake ya
filamu hiyo mpya ya SCOLA Bodi ya Filamu na ameahidi kurekebisha baadhi ya
vipengele kama alivyoelekezwa na Bodi hiyo kwani vitu hivyo vinaweza
kurekebishika.
Aunty Ezekiel
amefurahishwa sana na kuishurukuru Bodi ya Filamu Tanzania kwa kufanya
majadiliano mazuri juu ya filamu yake kwa kubaini mapungufu yaliyopo na
ameahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha filamu hiyo na pia amewaasa wasanii
wengine wote kuwa na imani na Bodi ya Filamu na kutokuwa na dhana tofauti juu
ya Bodi hiyo.
Aunty Ezekiel ni msanii
aliyetengeneza filamu nyingi hapa nchini ambazo zinasambazwa na Kampuni ya
Steps Entertainment iliyopo hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment