Kampuni
ya bia ya Serengeti katika juhudi zake za kutambua na kuthamini wateja
wake, leo imezindua promosheni ambayo inaendana na kampeni yake kuu
inayoendelea ya TUPO PAMOJA. Tupo Pamoja ni kampeni inayotambua wateja
na kusherehekea nao pamoja.
Mteja
anaweza kujishindia kuanzia shilingi elfu kumi hadi million moja na pia
anaweza kujipatia bia ya bure papo hapo. Kampeni hii inatarajiwa
kuendeshwa kwa miezi mitatu ijayo.
Katika
promosheni hii ya winda na ushinde, mteja atakaponunua bia ya
Serengeti ataweza kupata maelezo chini ya kizibo kama ilivyokuwa katika
kampeni iliyopita ya vumbua hazi na chini ya kizibo. Atapata namba
maalum ambayo atatuma kwa njia ya sms kwa namba maalum na papo hapo
atapata ujumbe utakaomjulisha ameshinda kiasi gani au kama amejipatia
bia ya bure.
Kama
kawaida ili kuhakikisha ushindi huu ni waukweli na uhakika, promosheni
hii itasimamiwa na bodi ya Bahati nasibu, kampuni maahiri ya PWC na
itaendeshwa na Push Mobile.
Akiwakaribisha
wageni na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuzindua promosheni
hii ya Winda na Ushinde iliyofanyika katika kiwanda cha kampuni hiyo
kilichopo Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya
Serengeti Ephraim Mafuru alisema kwamba bia ya Serengeti lager ni bia
inayojali na kuwatambua wateja wake kwa kiasi kikubwa.
“Kampeni
na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja
wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi. Bia hii
inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi,
tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya
wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au
nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
Uzinduzi
wa promosheni hii pia ulihudhuri wa na Mkurugenzi mkuu (Group Managing
Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu
(Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.
Wengine
waliohudhuria ni Maofisa kutoka bodi ya Bahati Nasibu, maofisawa PWC na
Push Mobile. Pia kutoa walihudhuria washindi waliowahi kushinda zawadi
mbalimbali katika promoshen za nyuma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Steve Gannon
akionesha namna ya kutuma ujume wa promosheni ya WINDA NA USHINDE kwa
kutuma ujumbe kupitia namba iliyowekwa maalum kwa promosheni hiyo,mbele
ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi
kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo.Pichani
kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na
mmoja washindi aitwaye Rahma,aliyewahi kujishindia piki piki kupitia
promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
0 comments:
Post a Comment