Nafasi Ya Matangazo

May 02, 2013



Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah na Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Ligi kuu ya Zanzibar,Consolata Adam.wakionesha kwa waandiushi wa habari (jhawapo pichani zawadi ya Kombe kwa Mshindi wa Kwanza wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar 2013/14,katika ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro House,Masaki jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitangaza zawadi kwa Mshindi wa Kwanza wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar 2013/14,katika ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro House,Masaki jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Ligi kuu ya Zanzibar,Consolata Adam.

 ******      ******
Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimelianika Kombe Kubwa litakalokabidhiwa kwa mshindi wa ligi kuu ya Zanzibar inayodhaminiwa na kinywaji hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa konesha kombe hilo, meneja Masoko wa kinywaji cha Grand Malt Bw. Fimbo Butallah alisema; Grand Malt ndiyo mdhamini mkuu wa ligi kuu Zanzibar, ijulikanayo kama “Grand Malt Premier League” na tumesaini mkataba wa udhamini kwa miaka mitatu, tangu mwaka 2012 ambao msimu wake wa ligi ndio unakamilika mwezi huu wa Mei.  Siku ya leo tumekutana hapa kushuhudia kombe hili lenye hadhi na heshima kubwa atakalokabidhiwa mshindi wa Ligi kuu ya Zanzibar siku ya Jumamosi tarehe 4 mwezi huu katika uwanja wa Amani, Zanzibar.

Kulingana na msimamo wa Ligi kuu ya Grand Malt, timu ambayo tayari imekwisha jihakikishia ubingwa ni KMKM ambayo siku ya Jumamosi itakuwa katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Zimamoto, na baada ya mchezo huo zitafuatia shamra shamra za mshindi kukabidhiwa kombe hili, ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Balozi Seif Ally Idd. Mshindi huyo pia atapata medali na kitita cha shilingi 10,000,000/- kama zawadi ya mshindi wa kwanza, wakati mshindi wa pili atapata medali na kitita cha shilingi 5,000,000/- toka kwa wadhamini, Grand Malt.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya shamra shamra hizo za siku ya Jumamosi, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam alisema; maandalizi yote yamekamilika, na Grand Malt imejipanga kuwapa burudani tosha wakazi wa Zanzibar kwani tumeandaa vikundi mbalimbali vitakavytoa burudani uwanjani tangu saa 7 mchana, ikiwemo vikundi vya sarakasi na ngoma maarufu ya “Kidumbati” hivyo tunawaomba watu wafike mapema uwanjani ili kuweza kupata burudani hizi. Na ninapenda kuwakumbusha mashabiki wa soka kuwa hakutakuwa na kiingilio katika mechi hiyo ya siku ya Jumamosi, hii ni siku maalum ya kila mtu kupata burudani hizi zilizoandaliwa na Grand Malt na pia kushuhudia mabingwa ambao wamefungua pazia kwa mara ya kwanza kutwaa kombe la ligi kuu ya Grand Malt.   

Posted by MROKI On Thursday, May 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo