Mtaalamu wa tiba viungo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Jackline Mariki akitoa elimu kuhusu afya bora mahala pa kazi wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya kwa wafanyakazi wa Boharai Kuu ya Dawa (MSD) iliyoanza leo katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce akimuonesha namna uwiano wa uzito na urefu unavyatakiwa kuwa Mfanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Christopher Komba wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya inayofanywa na wataalamu kutoka JKCI katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam.
27/01/2026 Wafanyakazi wanaotumia muda mwingi maofisini wametakiwa kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo shinikizo la juu la damu na magonjwa ya moyo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce akimuonesha namna uwiano wa uzito na urefu unavyatakiwa kuwa Mfanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Christopher Komba wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya inayofanywa na wataalamu kutoka JKCI katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya iliyoanza leo katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha na Khamis Mussa
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa afya iliyoanza leo katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha na Khamis Mussa
****************
Na Mwandishi
Maalumu - Dar es Salaam.27/01/2026 Wafanyakazi wanaotumia muda mwingi maofisini wametakiwa kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo shinikizo la juu la damu na magonjwa ya moyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Daktari bingwa wa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi wakati akitoa mafunzo maalumu kuhusu namna ya kuzuia magonjwa ya moyo na shinikizo la juu la damu katika kambi maalumu ya siku mbili ya upimaji wa afya kwa wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Akizungumzia hali ya afya nchini, Dkt. Theophilly alisema takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha kuwa asilimia 20 ya vijana nchini wanakabiliwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, huku upande wa watu wazima tatizo hilo likichukua asilimia 35%.
“Mazingira ya kazi za mijini, kushindwa kupata nafasi ya kufika katika vituo vya afya ili kufanya uchunguzi wa afya, kazi za kukaa muda mrefu ofisini bila mazoezi, vimechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya moyo miongoni mwa wafanyakazi wanaotumia muda mwingi ofisini”, alisema Dkt. Theophilly
“Magonjwa ya moyo na shikinizo la juu la damu yameendelea kuwa tishio kubwa kwa jamii hususani wafanyakazi wa mijini ndio maana leo tumefika MSD ili kutoa elimu ya afya bora mahali pa kazi, kufanya upimaji wa afya, kuwapa elumu kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi, kuzingatia uzito wenu wa mwili na kuzingatia lishe bora,” alisema Dkt. Theophilly.
Kwa upande wake Mtaalamu wa tiba viungo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Jackline Mariki alisema ni muhimu wafanyakazi wakazingatia afya mahali pa kazi ili kuepuka maumivu ya shingo mabega na mgongo yanayotokana na kukaa kwa muda mrefu na kutokukaa kama inavyotakiwa.
“Tumeona ni muhimu tukawaelimisha wafanyakazi kuhusu afya mahali pa kazi ili waweze kufahamu namna sahihi ya kukaa, aina ya viti vitakavyowaepusha kupata shida za mgongo, namna nzuri ya kunyanyua vitu na kupanga vifaa ili waweze kujikinga na magonjwa ya viungo vya mwili,” alisema Jackline.
Nao wafanyakazi wa MSD walisema mafunzo waliyoyapata yamewapa uelewa mpana kuhusu umuhimu wa kujali afya zao hivyo kuepuka kupata maradhi yanayoweza kuzuilika endapo hatua za kinga zitazingatiwa ipasavyo.
“Nawashukuru sana wataalamu wa JKCI kwa kutufiika na kutupa elimu ambayo itanisaidia kujikinga na magonjwa ya moyo, kinga ni bora kuliko tiba nitatumia elimu niliyoipata kufanya mazoezi yatakayoniepusha na magonjwa hayo,” alisema Emanuel Kiunga, Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
“Kama mfanyakazi ninayetumia muda mwingi kukaa ofisini nimejifunza kupangilia muda wangu ili niweze kupata na muda wa kuchunguza afya yangu na kujilinda na magonjwa yasiyoambukiza, pia nitazingatia ushauri tuliopewa na wataalamu ili afya yangu iwe imara wakati wote,” alisema Dorothy Mtatifikolo.









0 comments:
Post a Comment