Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Benki ya Barclays Tunu
Kavishe,akikabidhi hundi ya Sh 61 Milioni kwa Mkurugenzi wa Mradi wa
Chuo cha Utabibu Baylor Dk Lumumba Mwita(kushoto)wakati wa makabidhiano
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,ambapo fedha hizo zitasaidia
vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
**********
Benki ya Barclays Tanzania jijini- Dar Es Salaam imetangaza
udhamini wa shillingi za kitanzania milioni 61 (TZS 61,000,000) kusaidia klabu
ya Baylor Tanzania iliyoundwa kwa vijana wa umri wa kati wanaoiishi na virusi
vya ukimwi na sehemu ya Chuo cha Utabibu cha Baylor cha Mfuko wa Watoto
Tanzania (Baylor-Tanzania), asasi hiyo isiyo ya kiserikali, iliyosajiliwa chini
ya muungano kati ya serikali ya Tanzania, USAID na Chuo cha Utabibu cha Baylor.
Baylor
– Tanzania
hufanya kazi Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini, katika kituo cha kliniki ya
watoto (Children’s Clinical Centers of Excellence (COEs)) kilichopo Mwanza
(kilichojengwa kwa msaada wa Bristol Myers Squibb Fundation) na Mbeya
(kilichojengwa kwa msaada wa mfuko wa Abbott).
Baylor Tanzania ni sehemu ya
mtandao ulioenea Afrika: asasi hii anzilishi ya kimataifa ya kushughuikia masuala
ya ukimwi wa watoto (Baylor
International Pediatric AIDS Initiative (BIPAI)), huendesha vituo vya kliniki
za watoto na kliniki nyinginezo katika nchi kumi na mbili za jangwa la Sahara
Afrika na vile vile Romania, na inajishughulisha na kutoa huduma za kinga ya
afya ya mtoto, kimsingi HIV, kifua kikuu, malaria, ukosefu wa lishe na sababu
za kawaida zinazosababisha magonjwa ya watoto.
Watoto zaidi ya laki moja
(100,000) na watu wazima wameshazipokea huduma za BIPAI tangu mwaka 1996, na
kukifanya kuwa chuo kikuu kikubwa duniani kinachojihusisha na maendeleo ya afya
ya mtoto.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari leo, Bi. Tunu Kavishe, Mkuu wa
mawasiliano na Huduma za jamii wa
Barclays Tanzania amesema, “Benki ya Barclays hujali umuhimu wa uraia kwa
umakini na kutambua hilo kama ufunguo wetu wa kibiashara. Tunapendezwa kufanya
kazi pamoja na klabu ya vijana ya Baylor kuwapa nguvu vijana walioathirika na
virusi vya ukimwi (HIV) na kuwa na uelewa chanya, kukuza mioyo yao na
kuendeleza umuhimu wao kamili katika kupata ujuzi wa maisha, uzoefu mbalimbali,
umuhimu wa utu uzima wa kuigwa na kazi maalumu, mwishowe kuwaongoza kukuza
maendeleo yao ya kikliniki na kiakili katika muendelezo wa kuelekea utu uzima”.
Mkurugenzi wa mradi kutoka
Chuo cha Utabibu cha Baylor ambae hufanya kazi pamoja na vijana wa klabu Dk.
Lumumba Mwita alisema “kuwapa kinga madhubuti ya virusi vya ukimwi vijana
wanaopevuka huhitaji msaada mkubwa wa kijamii kutoka katika familia, vijana
wenye umri sawa na wao na watu wazima wa mfano - kuwashawishi tiba halisia,
kuwa wawazi, lishe bora na tabia nyingine za kiafya. Vijana wanaoishi na virusi
vya ukimwi (HIV) wana mahitaji yao
mahususi lakini mahitaji hayo maranyingi hayafikiwi kwa sababu mbalimbali
zikiwemo zile za kinga na mipango ya misaada ambayo mara nyingi hujengwa kwa
watu wazima na kwa afya za watoto.
Klabu ya Baylor hutoa elimu ya jinsi gani ya
kuishi na virusi vya ukimwi na huwaaminisha
walengwa kwamba kuna maisha ya kuishi dhidi ya virusi vya ukimwi. Pia
huwa ni sehemu ya kupata uhakiki, umri kamili wa kuanza mapenzi na maelezo ya
afya ya uzazi, ujuzi wa maisha ukiwemo uongozi na maendeleo, utoaji maamuzi,
kupambanua ujuzi, mawasiliano, miradi inayozalisha kipato cha ziada na mengine
mengi. Aliongezea “tungependa kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa Benki ya Barclays Tanzania kwa kutambua
umuhimu wa kufanya kazi na Baylor na kutusaidia katika fedha za kuendelea
kujiendesha na kuwapatia ujuzi sahihi vijana”.
Baylor
Tanzania
hivi sasa husaidia Klabu Wanachama za Vijana zaidi ya mia sita (600) Kanda ya
Ziwa na Nyanda za juu Kusini – namba hii inatarajiwa kuongezeka kadri watoto
wanaoishi na virusi vya ukimwi kutambuliwa, kuandikishwa katika tiba na kuishi
katika umri huo na zaidi.
0 comments:
Post a Comment