Mahmoud Ahmad Arusha.
Jeshi la polisi mkoani hapa
limefanikiwa kukamata magunia 30 ya bangi huku askari wawili wa jeshi hilo
mkoani hapa wakikamatwa wakati wakisindikiza magunia 18 ya madawa ya kulevya
aina ya mirungi kwenye mpaka wa nchi na Kenya Holili mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na vyombo vya
habari Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa kamishna wa msaidizi wa polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo tarehe 19 mwezi huu huko mpakani mwa nchi ya
Kenya na Tanzania Holili mkoani Kilimanjaro askari wawili wa Jeshi hilo mkoani
hapa Koplo Edward na Mwenzake PC.George walikimatwa akisindikiza mirungi
magunia kumi nane.
Kamanda Sabas alisema kuwa
watuhumiwa hao wapo mkoani Kilimanjaro na taarifa zao anazo kamanda wa polisi
mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alibainisha kuwa jeshi hilo limefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na bangi magunia 30 katika msako mkali
walioufanya kwenye kata ya Ngarenanyuki wilayani Meru.
Sabas alibainisha kuwa wengine
wawili walikimbia na jeshi hilo linawatafuta katika hatua nyingine jeshi hilo
limakamata gari lenye namba za usajili KBQ372V lililoibiwa nchi jirani ya Kenya
majira ya saa 6:30 usiku huko wilayani Longido.
Kamanda Sabas alisema kuwa
katika kupambana na mitandao ya madawa ya kulevya walifanikiwa kuwakamata
askari hao na kuwataka watanzania na wakazi wa mkoa huu kutoa taarifa
zitazosaidia kumaliza matukio ya kiuhalifu mkoani Arusha kwani Arusha bila ya
madawa ya kulevya inawezekana na nchi vile vile pia
0 comments:
Post a Comment