Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako amemtambulisha rasmi Mshambuliaji Mrisho Khalfan
Ngassa kuwa mchezaji mpya kujiunga na timu hiyo msimu ujao wa Ligi na michuano
ya kimataifa.
Mrisho Ngassa ambaye
anarudi Yanga baada ya kuihama timu hiyo kwa kutimkia kwa Matajiri wa Bongo,
Azam FC na baade mwaka jana kuzwa Simba kwa Mkopo baada ya kutokea sintofahamu
za kimaadili ndani ya Klabu yake hiyo.
Ngassa alienda
kuichezea Simba msimu uliopita baada ya Klabu yake ya Azam kuchukizwa na
kitendo chake cha kuibusu jezi ya Yanga wakati timu hizo zikicheza.
Ngassa anakuwa ni
mchezaji wa kwanza kuatangazwa na klabu hiyo kumsajili muda mfupi tu baada ya
kumalizika kwa Ligi Kuu na tayari ameshaanguka saini ya kuichezea klabu yake
hiyo ambayo anamapenzi nayo makubwa hapa nchini kwa miaka 2.
Mrisho
Ngassa akiibusu jezi ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi kurejea
katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili asubuhi ya leo, makao ya
klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment