Na Mwandishi Wetu
SHINDANO
la mkutafuta malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013"
litafanyika Juni 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani,Mkoani humo.
Akizungumza
na gazeti hili jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha
Kigundula, alisema kuwa warembo tayari wameanza mazoezi yakatofanyika
kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
Kigundula
alisema shindano hilo litaanza saa 2, usiku, ikiwa ni pamoja na kuwa na
burudani mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa nchini pamoja
na wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo.
Kigundula
alisema kuwa mpaka juzi warembo 10 wamejitokeza na kuanza mazoezi
yanayosimamiwa na Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.
Warembo
hao ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack
Emannuel (18),Waida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwanahamis
Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19)
na Aisha Rashid (21).
"Kila
kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha
kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina
yake"alisema Kigundula
Alisema
kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani
humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya
urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.
Redd's
Miss Tanga 2013 imedhaminiwa na Redd's Original,CXC Africa, Executive
Solutions,Busta General Supply, Mkwabi enterprises,Lusindic Investment
LTD, Lavida Pub, Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers,Cloud's Media
Group,Michuzi Media Group na Blogs za Bongostaz.com, Saluti5, Kajuna,
JaneJohn, na Father Kidevu Blog.
0 comments:
Post a Comment