Balozi
wa Airtel nchini Ambwene Yessaya (AY) (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na wanafunzi wa chekechea ya shule ya msingi Buguruni Viziwi
walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii.Airtel kwa kushirikiana
na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye
uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia.
Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiangalia ujuzi wa wanafunzi wa
shule ya Buguruni viziwa alipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii.
wakati AIRTEL na Balozi wao msanii AY walipofanya ziara maalum ya
kuhamasisha jamii kuchangia wanafunzi hao wa shule ya msingi Buguruni
viziwi kupata vifaa vya kujifunzia kwa kushirikiana na BAMVITA.
Mwalimu
wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule
hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni
mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeromia, akifuatiwa na Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene
Yessaya (AY). Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi
maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya
kujifunzia
Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya
Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea
shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia
pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu
unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu
wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador
ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi.
Winfrid Jeromia.
****
Ni moja kati ya shule zitakazofaidika na mradi wa Airtel na BAMVITA
Wanafunzi wa shule ya Buruguni viziwi wameomba watanzania na wadau mbalimbali kuchangia ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA. Wanafunzi hao waliosema hayo wakati Airtel pamoja na balozi wake AY walipotembelea shuleni hapo mwisho mwa wiki hii.
Wanafunzi wa shule ya buruguni viziwi ambao mbali na masomo ya darasani pia wanafundishwa kazi za stadi, walionekana kufanya kazi za stadi za mikono ikiwemo kutengeneza shanga pamoja na mazulia madogo ya miguu, wametia hamasa na kuthibithisha kwamba wakiwezeshwa na kupatiwa nyenzo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya shughuli za stadi na ubunifu.
Akiongea katika ziara hiyo Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema “leo tumetembelea shuleni hapa ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wetu katika kubainisha mahitaji ya ziada ambazo shule hizi zenye mahitaji maalumu zinahitaji. Shule ya Buruguni viziwi ni moja kati ya shule zitakazofaidika Mradi huu unaoshirikisha Airtel na BAMVITA una lengo la kusaidia kuendeleza kiwango cha Elimu hapa nchini na kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza kushiriki na kuchangi elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum. ‘
Naye Balozi wa Airtel AY Ambwene Yesaya alisema “ Tunawashukuru watanzania kwa kuitikia wito na kuanza kuchanga na tunaendelea kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 au kuchangi kiwango chochote kupitia Airtel money 0788 041361 ambapo jina la fumbo ni VITABU.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi bi. Winfrid Jeromia alikuwa na haya ya kusema”tunaishukuru sana Airtel kwa kuweza kuja na mradi kama huu wa kuweza kuinua Elimu hapa nchini na kurahisha mazingira yetu ya ufundishaji hapa shuleni. Tunawaomba watanzania wengine na makampuni mengine makubwa yajitokeze kwa wingi kuweza kuchangia katika mradi huu ili kuinua wigo wa Elimu hapa nchini.
Kampeni hii ya kuchangia vifaa kwa shule zenye mahitaji maalumu inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana ilizinduliwa Agosti 23 2012 na itaendelea kwa muda kwa mienzi mitatu. Kwa kuanzia shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Uhuru Mchanganyiko, Sinza Maalum, na Buguruni Viziwi zitafaidiaka na mradi huu.
0 comments:
Post a Comment