Mkuu wa
Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Towo Kavishe (kushoto)
akionyesha jezi halisi ya timu ya Manchester ikiwa ni moja ya zawadi
watakazopewa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL)
inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia
tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo
nchini Uingereza. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia
ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bakari
Maggid na Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu.
Mkazi wa
Jiji la Dar es Salaam, Rukia Kizwi (kushoto) akitoa tiketi ili kumpata
mmoja wa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL)
inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia
tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo
nchini Uingereza na wengine wawili hujishindia zawadi ndogondogo. Droo
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni
Mkuu wa Mawasiliano wa Barclays, Tunu Towo Kavishe, Mkuu wa Bidhaa,
Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu, Mkaguzi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid na Ofisa Mawasiliano wa Barlclays, Lilian Machera.
0 comments:
Post a Comment