Wahudumu mbali mbalimbali wa
Baa nchini, leo watapata mafunzo maalum ya jinsi ya kuwahudumia wateja
wanaotumia pombe kali (whiski) kutoka kwa balozi wa balozi wa kinywaji cha
Glenmorangie, Niel Hendriksz.
Mafunzo hayo yanalenga
upatikanaji wa huduma bora sambamba na uchanganyaji wa kinywaji hicho kwa lengo
la kuwafanya wanywaji kupata kinywaji kilicho bora kwa afya zao.
Akizungumza jijini jana,
Hendriksz ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku mbili alisema kuwa
wameamua kufanya mafunzo hayo ili kuboresha huduma zao na ni njia moja ya
kuboresha soko la kinywaji hicho hapa nchini.
Alisema kuwa bidhaa zao
zinatengenezwa nchini Scotland, na wamedumu kwa kipindi kirefu katika soko na
sasa wameamua kuongeza nguvu kwa upande wa hudhuma.
Mbali na kutoa mafunzo hayo,
barozi huyo atawaelimisha wahudumu hao juu ya uelewa kuhusu utumiaji wa
vinywaji hivyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema kuwa kwenye ziara ya
siku tano katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo hapa nchini
atakuwa kwa siku mbili na maunzo mengine atayatoa nchi nyingine.
Alifafanua kuwa atakutana na
makundi tofauti ya utoaji wa huduma ya kinywaji chao mbali ya wafanya boashara
mbali mbali lwa lengo la kudumisha soko.
“Kutakuwa na nafasi 20 kwa
nchi nzima kuhudhuria mafunzo ambapo pia tutabadilishana mawazo na watu mbali
mbali ambao ni wadau wa kinywaji chetu," alisema.
Ziara ya Hendrisksz
inatarajia kumalizika keshokutwa ambapo ataelekea nchini Nairobi kwa
mwendelezo wa ziara hiyo Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment