Nafasi Ya Matangazo

October 21, 2012

 Na Mwaandishi Wetu
Bandari ya Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa jumla katika michezo ya inter-ports games ambayoimefanyikajijiniMwanzahivikaribuninakufungwanaMkuuwaWilayayaNyamagana, Mh. Baraka Konisaga.

Michezohiyoimefanyikajijinihukokwamudawasikutanoambapozaidiyawanamichezo 400 wafanyakaziwaBandariwalishirikimichezombalimbalikama vile mpirawamiguu, pete, kikapu, riadha, baonakuvutakamba.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe na zawadi nyingine kwa wanamichezo hao, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana aliwaasa wanabandari kuendelea kushiriki michezo kwa ajili ya kujengaafyazaolakinikubwazaidikutekelezamajukumuyaoyakilasiikukwaufanisi.

“Leo isiwe mwisho wa kushiriki michezo endeleeni kushiriki ili kuoboresha afya zenu lakini pia niwashauri kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na mkumbuke kwamba mmepewa dhamana kubwa na taifa lenu hivyo ni wajibu wenukufanyakazikwabidiinakwauadilifumkubwa,”amesemaKonisaga.

Katika michezo hiyo Bandari ya Dar es Salaam iliibuka na vikombe vingi aidiambapo katikampirawasokawaliibukawashindiwa kwanza wakujinyakuliaalamanyingihukunafasiyapiliikichukuliwanaMakaoMakuu.

Kwa upandewampirawapetemshindiniBandariya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Katika mchezo wa kikapu nafasi ya kwanza ilikwenda Makao Makuu wakati Bandari Tanga wakinyakua nafasi ya pili.

Nafasi ya kwanza ya mchezo wa kuvuta kamba wanaume ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Mchezo wa kamba wanawake nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Tanga ilishika nafasi ya pili.

Kwa upande wa riadha Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena kidedea huku Bandari ya Tanga ikishika nafasi ya pili. Kwa upande wa wakimbiaji mita mia moja kwa wanawake medali ya dhahabu ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Makao Makuu, medali ya fedhailikwenda kwa mkimbiaji wa Bandari ya Tanga na mshindi wa tatu alikuwa mkibiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam aliyeibuka na medali ya shaba.

Kwa upande wa wakimbiaji wa mita mia moja wanaume medali ya dhahabu ilichukuliwa na mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam, fedha mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Bandari za Maziwa (Mwanza, Kigoma na Kyela).

Kwa upande wa mita mia nne wanawake dhabau ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam, fedha ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji wa Makao Makuu. Kwa upande wa mita mia nne wanaume dhahabu ilikwenda Tanga, fedha ilikwenda Makao Makuu na shaba ilinyakuliwa na Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wa mchezo mkongwe na wa jadi maarufu kama bao, Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena na ushindi wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Bandari ya Tanga.Kwaupandewawachezaji bora wakilamchezo, mlindamlangomahiriwatimuyaMtwara, Douglas Bahati aliibuka mshindi.

Kwa upande wamchezowampirawapete, MatalenaMhagamaambayepianimchezajiwatimuya taifa aliibuka kidedea na nafasi ya kwanza. Kwa upande wa timu bora ya kuvuta kamba Makao Makuu waliibuka naushindihukuBandariyaMtwaraikiibukanaushindiwatimu bora ya kuvuta kamba wanaume.

Mchezaji bora wariadhani Lucy Kyom akutoka Bandari ya Dar es Salaam. Bandari zilizoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Bandari Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu yenyewe. Michezo hiyo hufanyika mara moja kila mwaka kwa kuwashirikisha wanabandari na hufanyika mara moja kwa kila kituo.







Posted by MROKI On Sunday, October 21, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo