Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya awali
ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127
wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad
Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada.
Afisa
wa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada Joseph Sokoine akimkabidhi Mhe.
Spika taarifa ya maandalizi ya mkutano huo pamoja na hali ya kisiasa
ilivyo nchini Canada baada ya kuwasili kuhudhuria Mkutano wa 127 wa
Chama cha Mabunge Duniani (IPU).
|
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na wasaidizi wake, akiwasili
katika uwanja wa ndege mjini Quebec, Canada Oktoba 20. 2012. tayari kwa
kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha Mabunge Duniani, (IPU),
uliotarajia kufunguliwa rasmi leo Jumapili Oktoba 21, 2012, na
kumalizika Oktoba 26. Makinda ameongoza ujumbe wa wabunge wanne kutoka
Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani wakiongoza ujumbe
wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano huo.(Picha zote na Owen Mwandumbya wa Ofisi ya Bunge).
|
0 comments:
Post a Comment