Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, (Kulia), akipokea ripoti ya
uchunguzi wa kashfa ya wizi na madudu mengine kwenye bandari ya Dar es
Salaam, kutoka kwa mwenyekiti wa kamati iliyochunguza "madudu" hayo,
Bernard Mbakileki, ofisini kwa waziri jijini Dar es Salaam Jumapili
Oktoba 21, 2012. Kwa mujibu wa Mbakileki, ripoti hiyo ya
kurasa 285, imegundua mambo kadhaa :machafu" na imetoa mapendekezo
kadhaa ya hatua za kuchukuliwa ambapo waziri mwenye dhamana amewaahidi
watanzania kuwa taarifa ya hatua zitakazochukluliwa kufuatia ripoti
hiyo, zitatolewa Desemba mwaka huu wa 2012 ambapo amewataka Watanzania
kuvuta subira kwani kuanzia sasa, yeyote anayefanya kazi Bandarini,
akithubutu kunyofoa kitu basi nayeye atanyofolewa. Banadari
ya Dar es Salaam, imekuwa kwenye shutuma nyingi, ikiwemo kuchelewesha
mizigo ya wateja, urasimu lakini baya zaidi wizi uliokithiri wa mizigo
ya wateja. Waziri Mwakyembe
aliunda kamati hiyo kuchunguza tuhuma hizo kufuatia hatua yake ya
kumnsimamisha kazi, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari hiyo, Ephraem
Mgawe na wasaidizi wake |
0 comments:
Post a Comment