Nafasi Ya Matangazo

October 18, 2012

 Hakika si kila ajali itokeayo barabarani husikitisha bali zipo ambazo pindi zinapotokea watu hufurahi na kustaajabu vile ajali ilivyotokea. Hivi ndivyo ilivyolikumba gari hilo dogo Toyota Spacio T 629BRL iliyokuwa ikitokea maeneo ya Uwanja wa Ndege kuelekea mjinui na kupinduliwa kama inavyoonekana katika picha katika barabara ya Nyerere karibu na kituo cha Tazara jijini Dar es Salaam jana alasiri.
 Mashuhuda wa ajali hii wanapasha kuwa waluiona kama mchezo wa sinema gari hii ilivyokuwa ikipinduka kiasi hata dereva wake kuto kutambua na kushtuka gari ipo chali. Mashuhuda hao wanap[asha kuwa chanzo ni kuopigwa pasi na lori la mizigo.
 Wanadai kuwa baada ya kupigwa pasi gari hilo dogo lilinasa katika ngao ya lori hilo na taratibu wakati yanaenda katika foleni basi walishtukia gari ikigeuzwa ilikotokea na mara wakashangaa matairi yapo hewani.
 Polisi usalama barabarani walifika na kuchukua maelezo ya ajali na kisha kuomba wenuyenguvu walinyanyue gari hilo ili kuepusha msongamano barabarani.
 Walijitokeza watu na kulinyanyua gari hilo ambalo liliharibika vibatya upande mmoja ambao ulipigwa pasi kisha kuruka sarakasi.
Dereva wa gari hilo (shati nyeupe) hakupata madhara zaidi ya nae kustaajabu kulicho tokea.
Posted by MROKI On Thursday, October 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo