Nafasi Ya Matangazo

June 14, 2012

Mshindi wa taji la urembo kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'MissKigamboni City 2012' atazawadiwa shilingi 500,000 katika shindano litakalofanyika kesho  katika ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika  na warembo wote wako tayari kwa shinda o hilo.

Mratibu huyo amesema kuwa mshindi wa pili atazawadiwa  shilingi laki tatu na nusu, mshindi wa tatu shilingi laki tatu na washindi wa nne na watano wataondoka na kitita cha shilingi laki mbili kila mmoja huku kifuta jasho kwa warembo wengine saba waliobakia kitakuwa ni shilingilaki moja na hamsini ambapo jumla ya zawadi zote ni shilingili milioni mbili na laki tatu. 
Mgeni rasmi katika shindano hilo atakuwa ni diwani wa kata ya Kigamboni, DOTTO MSAWA ambaye  ametoa mchango mkubwa katika kufanikisha shindano hilo.
 Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
 "Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe mwenyewe," alisema mratibu huyo. 
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah,Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Winnie Karaya.

Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM na Kitwe Traders.
 
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
Posted by MROKI On Thursday, June 14, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo