Nafasi Ya Matangazo

April 30, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
 
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa ka furaha na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyaakzi Tanzania (TUCTA) Bw Nicholaus Mgaya  leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
 
: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
Rais Jakaya Mrisho Kikweteakiwapungia mkono  mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Hani Abdalla Mohammed  Mu'minah,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar jana kujitambulisha kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Nchini Tanzania Mohsen Movahhed Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar jana kwa mazungumzo na  Rais.
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments
 Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati walipofanya mazoezi ya pamoja jana.
WAREMBO wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja katika kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani ya urembo.

Warembo wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.

Vitongoji vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss Tanzania 2012.

Wakizungumza jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa kati wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.

“Tunawashukuiru sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali ambao ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.

Nae Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na kufnya nao mazoezi ya pamoja.

Mapema Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.

Shindano la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.
 Miss Ukonga 2012 wakicheza mziki wa ufunguzi
 Baadhi ya waremnbo wa Tabata wakipita kwa mwendo wa madaha.
Warembo Ukonga wakicheza ngoma.
Warembo wa Miss Ukonga 2012 wakimwangalia Mshiriki mwenzao kutoka Tabata akipita mbele yao.
Ngoma ya asili nayo imo na hapa ni kucheza kwenda mbele.
Mwandaaji wa Miss Tabata, Freddy Ogot (katikati) akiwaeleza jambo waandaaji wa Miss Ukonga 2012.
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments
MVUA kubwa zinataraji kunyesha katika kipindi cha saa 24 kila siku katika mikoa nane nchini kuanzia leo Aprili 30 hadi Mei 4, mwaka huu.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 30, 2012 Asubuhi na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zinasema kuwa mvua hiyo kubwa ya zaidi ya milimita 50 itanyesha kila siku katika siku hizo zilizotajwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa 8 nchini ya ukwanda wa Pwani.

Aidha TMA hiyo inasema kuwa kiwango cha uhakika cha mvbua zitakazo nyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Morogoro, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba itakuwa ni asilimia 80.

TMA inaeleza kuwa mvua hizo ni kutokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa  hali ya hewa katika maeneo ya Bahari ya Hindi yanayopakana na Pwani ya Kaskazini.

Kufuatia mvua hizo TMA wanasema upo uwezekano mkubwa wakutokea Mafuriko, Tsunami, upepo mkali, mchafuko wa bahari na maziwa, vimbunga , Baridi kali au joto.

Tahadhari kubwa imetolewa kwa wakazi wote wanaoishi maeneo hatarishi kama mabondeni na karibu na mito mikubwa kwani panauwezekano mkubwa wa kutokea mafuriko kufuatia mvua hizo.

Pia tahadhari hiyo itawahusu watumiaji wa Bahari na nchi kavu na kutakiwa kuchukua tahadhari juu ya athari zitokanazo na mvua hizo.

TMA pia imezitaka taasisi zinazohusika na maafa kuchukua hatua stahiki mapema kabola ya madhara makubwa kutokea na kuikumba jamii.

Mamlaka itaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa kila inapobidi.
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments
Serengeti Breweries Limited (SBL) is pleased to announce the appointment of Mr. Steve Gannon as Managing Director, effective 1 July 2012. Mr. Steve Gannon joins SBL from Diageo Cameroon Hub where he has been Managing Director since 2009. In this role at the helm of SBL, Mr. Gannon will be a member of the East African Breweries Ltd Executive committee.

Under Mr. Gannon’s leadership for three years, the Diageo Cameroun Hub business has delivered significant share growth in beer and established new businesses in premium spirits. During Mr. Steve Gannon’s tenure leading the Diageo Cameroun Hub business he has led significant investment behind building capacity and expanding the businesses routes to market. 

In addition, Mr. Gannon has been central in leading the development of the Business Coalition Against Corruption in Cameroon – an unprecedented initiative in partnership with the Cameroon government to create a private sector movement united against corruption. 

Prior to his role within Diageo Cameroun Hub, Mr. Steve Gannon has had 30 years commercial experience in Diageo, including leading the Diageo Venture Africa Business, launching the Guinness brand in a number of African markets as well as doubling the Diageo Africa spirits business in the Diageo Venture Africa markets.
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments
Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa kwa sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.
 
Akizungumza wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Oyesterbay Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu na utawala bi Jane nchimbi alisema 'Tumekuwa na utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa tumebanwa na majukumu ,lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuufanya utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa umma  tunatumia muda mwingi kwenye ofisini tukihudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi kama ambavyo NHIF tumethubutu...
 
Mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi  za Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi (gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.alisema Bi Jane kijazi
 
Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete  ya NHIF bi Sabina Komba  ……aliwataka wafanyakazi wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi mengi na  makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments
Mwanahabari Alein Philip wa Ebony Fm ,Happines Matanzi wa Tanzania daima Iringa ,Paulina Kuye wa Nuru na Laurian Mkumbata wa ITV wakivuta daraja la mto Mdonya katika hifadhi ya Ruaha
Wanahabari wakivuka daraja la kamba ya mto Udonya katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha hakika ni zaidi ya utalii iwapo utafika hifadhi ya Ruaha Iringa
Mwanahabari wa radio Country Fm Iringa Sophia Mpunga (kushoto ) akiwa na mwandishi wa radio Nuru Fm Mahija Zayumba katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha huku nyuma yao kukiwa na twiga
Mwanahabari Paulina Kuye wa Nuru FM akipiga picha na Twiga katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa ziara ya wanahabari mkoa wa Iringa katika hifadhi hiyo ya Ruaha
Wataka kujua dhidi ya Swala ?
Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Iringa Laurian Mkumbata akijiweka sawa kwa kuchukua matukio katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya ziara ya siku tatu ya kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi hiyo kubwa kuliko zote Tanzania
Mwandishi wa habari wa Nipashe Iringa VickyMacha akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa hifadhi Bw Marando
Madereva wa gari la wanahabari wakishangaa wanyama katika hifadhi hiyo ya Ruaha
Wanahabari mkoani Iringa wameanza kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi ya Ruaha kama njia ya kuwahamasisha zaidi watanzania kupinda kutembelea hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ambayo ni hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ila pia kuhamasisha utalii katika hifadhi za mikoa ya kusini ikiwemo ya Kitulo, Katavi na Ruaha ambazo bado zipo nyumba kwa uhamasishaji. Picha zote na Francis Godwin
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Saruji 143 kwa Sheha wa Michenzani  Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani  ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiawani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Wakwanza kulia ni sheha wa Stahabu-pemba bw haji Faki Kombo na kati ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari. 
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa mabati 264 kwa sheha wa Stahabu-pemba bw haji Faki Komb  ikiwa ni msaada wa Airtel kushiriki kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Kati mwenye shati la drafti akishudia ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari na anaefuata ni Sheha wa Michenzani Bw Abdalah Omari.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa Nondao 62 kwa Sheha wa Michenzani  Mzee Abdalah Omari huko Pemba visiwani  ikiwa ni msaada wa Airtel kushirikiana na wananchi wa Tanzania visiawani kwaajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya kuhudumia familia mbali mbali  za maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa wiki. Naeshudia kati  mwenye shati la drafti ni Afisa Mipango wa Wilaya Mkoani Bw Omar Shehe Omari
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari pamoja na wananchi huko pemba mara baada ya kukabidhimsaada wa Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo ili kuboresha huduma za afya katika maene ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu, Kandandarani na Shidi huko pemba mwishoni mwa wiki

********
  • Kituo hicho kitafaidisha zaidi ya watu 9,000 wa maeneo ya Bogoa, Shidi na  Michenzani
  • Airtel yakabidhidhi Mabati 264,  Saruji 143, Nondo 62 na Mbao za kupau kituo cha Afya Michenzani
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbali mbali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kisiwani pemba maeneo ya michenzani kitakachosaidia kutoa huduma maeneo ya  STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa Airtel Zanzibar Bw Hagai Samson alisema “msaada huu wa Airtel kwa wakazi wa huku pemba hautaishia hapa , leo tumejitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha afya tukiwa na imani vikitumika kwa usahihi vitasaidia kuboresha huduma za afya katika maene ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu, Kandandarani na Shidi.

Airtel Tanzania tunawashukuru sana wateja wetu mliopo pemba kwa kuwa ndio hasa wanaotuunganisha na jamii hii siku ya leo. Tunachojitolea hapa ni sehemu ya faida tunayoipata kila mnapozitumia huduma zetu zikiwepo kupiga na kupokea simu, Airtel money pamoja na huduma yetu ya Internet ya  3.75G.

Kwa upande wake Sheha wa Michenzani akipokea  msaada huo wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho cha Afya aliishukuru Airtel na kuwaomba wadau wengine wanaofanya biashara kisiwani huko kuiga mfano huo wa Airtel.

“ naishukuru sana Airtel kwa msaada wao huu, utatusaidia sana kukamilisha ujenzi wa  kituo hiki cha Afya hapa michenzani, tunaamini hii ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Ally M. Shein  ambae wiki moja iliopita aliweka jiwe la msingi katika kituo hichi na kuhimiza  ujenzi wa kituo hiki uende kwa kasi ili kusaidia kupunguza adha ya mrundikano wa wagonywa katika kituo kimoja kile cha Bogoa.

Nae Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani Omari Shehe Omari akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya una lengo la kupunguza matatizo ya afya yanayoikabili jamii inayoishi maeneo hayo hasa kwa kuzingatia wakina mama na watoto.

“Ninaipongeza Airtel sana kwa kujitolea na kutusaidia kufikia malengo yetu ya Milenia, sisi tuna dhamira ya kuboresha Afya na elimu kwa pamoja, kila Skuli iwe na kituo cha Afya au kila Shehia  (Serikali ya Mtaa) iwe na kituo chake cha Afya.

Hivyo kwa msaaada huu utasaidia sana serikali yetu kutifika malengo yake kwamba pia michenzani watapata kituo chao hapa karibu.” Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ina mkakati wa kutoa misaada ya kijamii kwa kugusa sekta za mazingira, Elimu na Afya kwa  lengo la kuisaidia serikali na jamii kwa ujumla kupambana na changamoto mbalimbali .

Mwaka huu wa 2012 pia Airtel  imejipanga kuhakikisha jamii iliyopo pembezoni mwa nchi mbali na kupata huduma bora ya mawasiliano ikiwemo ile ya Airtel money pia itashiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ili kujenga vyema ushirikiano na jamii kama ilivyoshiriki kuboresha miundombinu ya Afya  Visiwani Zanzibar.
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2012 No comments

April 29, 2012

  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Al Ahly Shandy, huku mchezaji wa timu hiyo Isaac Seun Malik,  akijaribu kumzuia katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo na Simba kutoka kifua mbele kwa goli 3-0.

Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Patrick Mafisango, Uhuru Selemani na Emmanuel Okwi, hata hivyo mchezji Patrick Mafisango alikosa goli la penati baada ya mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa vibaya na beki wa timu ya Al Ahly Shandy katika kipindi cha kwanza. Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo nchini Sudan.
Picha na Fullshangwe Blog.
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments
Msanii AT akibambia vilivyo katika Show ya Washindi wa Tuzo za Kilimanjaro hapo jana Katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma
Mwanadada aliyeteka mioyo ya watu kwa kukata mauno wakati alipopanda stejini kwenye show ya washindi wa Tuzo Za Kilimanjaro Music iliyofanyika Jana katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma
Alikiba akiwa na Wacheza show wake katika show hiyo ya kili music awards iliyofanyika jana Mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri
 Diamond & Ommy Dimpoz
Umati wa Wakazi wa Dodoma Wakiwa Kwa Wingi Katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma Hapo Jana katika Show ya Washindi wa Kili Music Award 2012 
 Umati wa Wakazi wa Dodoma na Vitongoji Vyake wakiwa kwenye Show ya Washindi wa Tuzo za Kili Music Awards iliyofanyika Jana katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Picha na Josephatlukaza Blog
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments
Cheka akivishwa Mkanda wa IBF na Meya wa Ilala, Jerry Slaa.
 
HATIMAYE kitendawili cha nani ataibuka Bingwa wa IBF kati ya mabondia Francis Cheka na Mada Maugo kimefikia kilele hapo jana katika ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam baada ya Cheka kushinda kwa TKO pambanano hilo.

Pambano hilo la raundi 12 lilifikia tamati katika Raundi ya 6 kabla ya kuingia raundi ya 7 baada ya Mada Maugo aliyekuwa akicheza katika uwanja wake wa nyumbani kuzidiwa na masumbwi ya Fransic Cheka wa Morogoro na kushindwa kuingia ulingoni.


Ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Mada Maugo alitangaza kutoendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi huku akisikika kusema, 'Sirudi Jamaa ataniua' huku akivua Glovz na kumpa ushindi mpinzani wake wa Teknical Know Count TKO. 
Mada aliomba kusitishwa kwa pambanano hilo lililokuwa la uzito wa KG 75 hivyo kumpa ubingwa wa IBF pamoja na gari Francis Cheka na kukata kabisa majagambo ya mada Maugo. 

Katika Historia ya wanamasumbwi hao hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.

Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.

 Pambano hilo liliandaliwa na Kampuni ya KITWWE GENERAL TRADERS  na kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wakitoka Zambia na Uganda.
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments
Basi mali ya Kampuni ya HOOD likiwa limeacha njia na kuingia porini baada ya kupta ajali katika maeneo ya Mlima nyoka mkoani Mbeya. Basi hilo lililokuwa likitokea Jijini Mbeya kuelekea kati ya Arusha na Dar es Salaam lilipata ajali hiyo leo asubuhi baada ya kudaiwa kugonga gari lingine kwa nyuma na kuingia porini. Mashuhuda wanasema abiria kadhaa walipata majeraha madogo na mishtuko na hakuna aliyepoteza maisha. 
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments
 Mwana Libeneke mwenzetu ,Haki Ngowi na Edna Kyando wakiwa katika nyuso za furaja mara baada kumemeremeta vilivyo katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam na kuhitimisha siku yao kuu kwa mnuso wa nguvu katika hoteli ya Golden Tulip.Jiachie Blog inawatakia kila lakheri katika safari yenu ya maisha mapya mliyoyaanzisha,Mungu awape nguvu,uvumilivu,anama na upendo katika kila jambo.
Picha zaidi Bofya hapa
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments

Picha ya pamoja kati ya wahariri mbalimbali walioshiriki katika semina hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (wa kwanza kulia aliyechuchumaa)
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Nevilli Meena (kushoto) akijadiliana jambo na Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi. Kulia ni mmoja wa maofisa wa TGNP kutoka kitengo cha Habari.
Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wahariri katika semina hiyo
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam. 

Na Ripota Wetu.

MTANDO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa maoni ya jumla ambayo wangependa yaingizwe kwenye mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya ya Tanzania. Maoni hayo yalitolewa na TGNP kwenye semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika semina hiyo, Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi alisema madaraka katika muhimili wa utawala wa sasa ni makubwa hivyo kushauri yapunguzwe na kuwe na utengano kati ya mihimili  mikuu mitatu ya nchi.

Bi. Liundi pia ametaka uwepo wa uwiano sawa wa kijinsia (50/50) huku akitaka mawaziri wasiwe wabunge na uwepo wa utaratibu wa viongozi (wabunge, madiwani) kuwajibishwa katikati ya mihula tofauti na ilivyo sasa.

Aidha mambo mengine ambayo Bi. Liundi ameyatoa kama changamoto na kushauri yaingizwe kwenye mchakato wa Katiba Mpya ni pamoja na kufutwa kwa adhabu, uwepo wa uhuru wa kupinga matokeo ya urais baada ya kutangazwa na ukomo wa uongozi wa  wabunge, madiwani  na serikali za mitaa.

Amesema siasa za uliberali mamboleo zilizoletwa na  mataifa ya nje  katika nchi za kiafrika zimesababisha mtafaruku mkubwa katika siasa za kiafrika, hali ambayo imezua migomo na mapambano dhidi ya uporaji wa rasilimali, ubinafsishaji wa huduma za afya na kuzifanya kama bidhaa na uporaji mkubwa wa ardhi na madini.

“Harakati hizi zimesababisha makundi ya kijamii, vyama vya siasa na wanaharakati kuanza kudai mabadiliko ya katiba katika nchi zao. Mfano mzuri ni nchini Kenya 2007,” alisema.

Pamoja na hayo alisema licha ya mchango mkubwa unaotolewa na wanawake nchini Tanzania bado hakuna fursa sawa kimgawanyo wa masuala mbalimbali.

 Asilimia 80 ya nguvu kazi vijijini ni wanawake na asilimia 60 yao ni wazalishaji wa chakula. Wanawake ambao hawana ajira ni asilimia 40.3 (2006) ukilinganisha na wanaume ambao walikuwa asilimia 19.2 ( 2006), asilimia 66 ya wanawake wanafanya kazi zisizokuwa na kipato (kazi za huduma)... asilimia 39.5 ya wanawake hawajasoma ukilinganisha na asilimia 25.3 ya wanaume...,”

Awali akitoa mada katika semina hiyo ya wahariri, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya alisema licha ya uwepo wa maendeleo kwa kiasi fulani ukilinganisha na miaka ya nyuma, bado kuna mifumo kandamizi inayoikabili jamii ya kipato cha chini.

Alisema maendeleo ya huduma za jamii katika maeneo mbalimbali kwa kiasi kikubwa yanawanufaisha zaidi wenye nacho (matajiri) na si masikini. “Huduma za jamii zimeongezeka ndiyo lakini wanaonufaika zaidi na huduma hizo ni wachache...ukiangalia utaona Serikali inawajibika zaidi kwa wafadhili na si wananchi wake...,” alisema Bi. Mallya.

Alioneza kwa sasa hata tabaka la wasionacho na walionacho ni kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma huku jukumu la kuihudumia jamii likirudi kwa familia zenyewe (majumbani) na si Serikali walioiweka madarakani kuwahudumia wananchi wake. 
 Habari hii imeandaliwa na mtandao Thehabari.com (www.thehabari.com)
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo