Nafasi Ya Matangazo

April 29, 2012

Cheka akivishwa Mkanda wa IBF na Meya wa Ilala, Jerry Slaa.
 
HATIMAYE kitendawili cha nani ataibuka Bingwa wa IBF kati ya mabondia Francis Cheka na Mada Maugo kimefikia kilele hapo jana katika ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam baada ya Cheka kushinda kwa TKO pambanano hilo.

Pambano hilo la raundi 12 lilifikia tamati katika Raundi ya 6 kabla ya kuingia raundi ya 7 baada ya Mada Maugo aliyekuwa akicheza katika uwanja wake wa nyumbani kuzidiwa na masumbwi ya Fransic Cheka wa Morogoro na kushindwa kuingia ulingoni.


Ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Mada Maugo alitangaza kutoendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi huku akisikika kusema, 'Sirudi Jamaa ataniua' huku akivua Glovz na kumpa ushindi mpinzani wake wa Teknical Know Count TKO. 
Mada aliomba kusitishwa kwa pambanano hilo lililokuwa la uzito wa KG 75 hivyo kumpa ubingwa wa IBF pamoja na gari Francis Cheka na kukata kabisa majagambo ya mada Maugo. 

Katika Historia ya wanamasumbwi hao hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.

Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.

 Pambano hilo liliandaliwa na Kampuni ya KITWWE GENERAL TRADERS  na kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wakitoka Zambia na Uganda.
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo