Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Al Ahly Shandy,
huku mchezaji wa timu hiyo Isaac Seun Malik, akijaribu kumzuia katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo na Simba kutoka kifua mbele kwa goli 3-0.
Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Patrick Mafisango, Uhuru Selemani na Emmanuel Okwi, hata hivyo mchezji Patrick Mafisango alikosa goli la penati baada ya mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa vibaya na beki wa timu ya Al Ahly Shandy katika kipindi cha kwanza. Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo nchini Sudan.
Picha na Fullshangwe Blog.
0 comments:
Post a Comment