Picha
ya pamoja kati ya wahariri mbalimbali walioshiriki katika semina hiyo
na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (wa kwanza kulia
aliyechuchumaa)
Katibu
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Nevilli Meena (kushoto)
akijadiliana jambo na Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa
TGNP, Bi. Lilian Liundi. Kulia ni mmoja wa maofisa wa TGNP kutoka
kitengo cha Habari.
Mratibu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi (kulia)
akifafanua jambo kwa baadhi ya wahariri katika semina hiyo
Baadhi
ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina
iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana katika Hoteli ya
Protea jijini Dar es Salaam.
Na Ripota Wetu.
MTANDO
wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa maoni ya jumla ambayo wangependa
yaingizwe kwenye mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya ya Tanzania. Maoni
hayo yalitolewa na TGNP kwenye semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali
vya habari nchini.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam katika semina hiyo, Mratibu wa Kitengo cha
Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi alisema madaraka katika
muhimili wa utawala wa sasa ni makubwa hivyo kushauri yapunguzwe na
kuwe na utengano kati ya mihimili mikuu mitatu ya nchi.
Bi.
Liundi pia ametaka uwepo wa uwiano sawa wa kijinsia (50/50) huku
akitaka mawaziri wasiwe wabunge na uwepo wa utaratibu wa viongozi
(wabunge, madiwani) kuwajibishwa katikati ya mihula tofauti na ilivyo
sasa.
Aidha
mambo mengine ambayo Bi. Liundi ameyatoa kama changamoto na kushauri
yaingizwe kwenye mchakato wa Katiba Mpya ni pamoja na kufutwa kwa
adhabu, uwepo wa uhuru wa kupinga matokeo ya urais baada ya kutangazwa
na ukomo wa uongozi wa wabunge, madiwani na serikali za mitaa.
Amesema
siasa za uliberali mamboleo zilizoletwa na mataifa ya nje katika nchi
za kiafrika zimesababisha mtafaruku mkubwa katika siasa za kiafrika,
hali ambayo imezua migomo na mapambano dhidi ya uporaji wa rasilimali,
ubinafsishaji wa huduma za afya na kuzifanya kama bidhaa na uporaji
mkubwa wa ardhi na madini.
“Harakati
hizi zimesababisha makundi ya kijamii, vyama vya siasa na wanaharakati
kuanza kudai mabadiliko ya katiba katika nchi zao. Mfano mzuri ni nchini
Kenya 2007,” alisema.
Pamoja
na hayo alisema licha ya mchango mkubwa unaotolewa na wanawake nchini
Tanzania bado hakuna fursa sawa kimgawanyo wa masuala mbalimbali.
Asilimia
80 ya nguvu kazi vijijini ni wanawake na asilimia 60 yao ni wazalishaji
wa chakula. Wanawake ambao hawana ajira ni asilimia 40.3 (2006)
ukilinganisha na wanaume ambao walikuwa asilimia 19.2 ( 2006), asilimia
66 ya wanawake wanafanya kazi zisizokuwa na kipato (kazi za huduma)...
asilimia 39.5 ya wanawake hawajasoma ukilinganisha na asilimia 25.3 ya
wanaume...,”
Awali
akitoa mada katika semina hiyo ya wahariri, Mkurugenzi Mtendaji wa
TGNP, Usu Mallya alisema licha ya uwepo wa maendeleo kwa kiasi fulani
ukilinganisha na miaka ya nyuma, bado kuna mifumo kandamizi inayoikabili
jamii ya kipato cha chini.
Alisema
maendeleo ya huduma za jamii katika maeneo mbalimbali kwa kiasi kikubwa
yanawanufaisha zaidi wenye nacho (matajiri) na si masikini. “Huduma za
jamii zimeongezeka ndiyo lakini wanaonufaika zaidi na huduma hizo ni
wachache...ukiangalia utaona Serikali inawajibika zaidi kwa wafadhili na
si wananchi wake...,” alisema Bi. Mallya.
Alioneza
kwa sasa hata tabaka la wasionacho na walionacho ni kubwa ukilinganisha
na miaka ya nyuma huku jukumu la kuihudumia jamii likirudi kwa familia
zenyewe (majumbani) na si Serikali walioiweka madarakani kuwahudumia
wananchi wake.
Habari hii imeandaliwa na mtandao Thehabari.com (www.thehabari.com)
0 comments:
Post a Comment