Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa kwa sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.
Akizungumza wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Oyesterbay Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu na utawala bi Jane nchimbi alisema 'Tumekuwa na utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa tumebanwa na majukumu ,lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuufanya utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa umma tunatumia muda mwingi kwenye ofisini tukihudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi kama ambavyo NHIF tumethubutu...
Mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi za Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi (gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.alisema Bi Jane kijazi
Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NHIF bi Sabina Komba ……aliwataka wafanyakazi wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi mengi na makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi
0 comments:
Post a Comment