MVUA kubwa
zinataraji kunyesha katika kipindi cha saa 24 kila siku katika mikoa nane
nchini kuanzia leo Aprili 30 hadi Mei 4, mwaka huu.
Kwamujibu wa
taarifa iliyotolewa leo Aprili 30, 2012 Asubuhi na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zinasema
kuwa mvua hiyo kubwa ya zaidi ya milimita 50 itanyesha kila siku katika siku
hizo zilizotajwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa 8 nchini ya ukwanda wa
Pwani.
Aidha TMA hiyo
inasema kuwa kiwango cha uhakika cha mvbua zitakazo nyesha katika mikoa ya Dar
es salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Morogoro, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba
itakuwa ni asilimia 80.
TMA inaeleza
kuwa mvua hizo ni kutokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hali ya hewa katika maeneo ya Bahari ya Hindi
yanayopakana na Pwani ya Kaskazini.
Kufuatia mvua
hizo TMA wanasema upo uwezekano mkubwa wakutokea Mafuriko, Tsunami, upepo
mkali, mchafuko wa bahari na maziwa, vimbunga , Baridi kali au joto.
Tahadhari kubwa
imetolewa kwa wakazi wote wanaoishi maeneo hatarishi kama mabondeni na karibu
na mito mikubwa kwani panauwezekano mkubwa wa kutokea mafuriko kufuatia mvua
hizo.
Pia tahadhari
hiyo itawahusu watumiaji wa Bahari na nchi kavu na kutakiwa kuchukua tahadhari
juu ya athari zitokanazo na mvua hizo.
TMA pia
imezitaka taasisi zinazohusika na maafa kuchukua hatua stahiki mapema kabola ya
madhara makubwa kutokea na kuikumba jamii.
Mamlaka
itaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa kila inapobidi.
0 comments:
Post a Comment