Nafasi Ya Matangazo

March 04, 2012

 Cassian Ngamilo Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari juu ya Zimbabwe kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam.
Mabasi makubwa 44, aina ya Kinglong yalikuwa yamekwisha pakuliwa katika bandari hiyo kutoka China, kwa ajili ya safari ya Zimbabwe.
 BANDARI ya Dar es Salaam imeanza kuhudumia wateja wapya kutoka Zimbabwe na hivyo kufanya idadi ya nchi za nje zinazopitisha bidhaa katika eneo hilo kufikia tisa hadi sasa.

Kwa mujibu wa Meneja wa bandari hiyo, Cassian Ng’amilo, maendeleo hayo yanatokana na kuimarika kwa usalama wa mali za wateja, ufanisi pamoja na gharama za upakuaji wa mizigo zinazoridhisha.


Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam jana, Ng’amilo alisema, idadi ya magari yanayopitia bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 17 mwaka 2011, kutoka asilimia 14.5 mwaka 2005.


Wakati akisema hayo, mabasi makubwa 44, aina ya Kinglong yalikuwa yamekwisha pakuliwa katika bandari hiyo kutoka China, kwa ajili ya safari ya Zimbabwe.


“Wazimbabwe tuko nao sasa katika bandari yetu, walianza kupitisha magari madogo na sasa wanapitisha magari makubwa mengi. Hii ina maana kuwa wameridhika na bandari hii”.


Nchi nyingine zinazoitumia bandari hiyo ni Zambia, Burundi, Congo (DRC), Malawi, Rwanda, Uganda, Kenya, Msumbiji na Tanzania ambayo kwa sasa inaingiza asilimia 50 ya magari sawa

na nchi za nje zilizokuwa zikipitisha asilimia 40 pekee hapo awali.

Wakala wa upakuaji mabasi hayo ujulikanao kama Cosmos Haulage Co. ulisema kuwa uchaguzi wa bandari ya Dar es Salaam ulifikiwa baada ya kuilinganisha na ya Msumbiji na Afrika Kusini.
Posted by MROKI On Sunday, March 04, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo