Marehemu Jane Mponzi
Nivigumu kuamini katika mazingira ya kawaida...lakini Ukweli ni kuwa Jane Mponzi (Mrs Herry Makange) hatunaye tena duniani.Hakika ni kifo na msiba wa kustua sana, Jane amefariki ghafla kama alivyofariki Mume wake Herry Makange miaka kadhaa iliyopita.
Marehemu Jane amefariki leo Jumapili machi 4,2012 asubuhi kwa shinikizo la damu.
Mengi yanaweza kusemwa lakini Ukweli utabaki pale pale kuwa Jane hatunae tena. Nimajonzi kwa kila amjuaye na anaemfahamu Jane. Binafsi ni juzi tu nilizungumza nae kwa kutaniana mimi na yeye kama kawaida yetu tunavyotaniana mtu na shemeji yake. kumbe ilikuwa ni simu yangu ya mwisho kumpigia na kuongea nae...Jane pumzika kwa amani na Mungu akupe faraja ya milele na Msalimie sana rafiki yangu Herry Makange naimani amekupokea kwa furaha sana.
Blogu hii inatoa pole kwa Mtoto wako kipenzi, Familia ya Mzee Mponzi, Ndugu jamaa na marafiki zako wote na familia nzima ya Vodacom Tanzania.
Buruani Jane Mponzi.






Rest in Peace Jane, poleni sana familia ya Mponzi & Makange kwa msiba wa mpendwa wetu... Tutakukumbuka daima - Jarudi Nyakongeza
ReplyDeleteJamani Jane tutakumiss sana. You were such a lively person. I fell in love with your beautiful heart the first time we met. May the Almighty keep you in a beautiful place. Buriani Jane.
ReplyDeleteKwaheri Jane Mpozni, we had a quality discussion a few days ago. promise to accomplish all that we discussed. I pray for you & play for us!!
ReplyDeleteMay God, the almighty, rest your soul in eternal peace. Amen!!
Poleni sana wote mlioguswa na msiba wa Jane. Ila napenda kutoa maoni yangu kidogo kuhusiana na kauli ya kusema kwamba "Amsalimie mumewe huko, na bila shaka kampokea kwa shangwe sana". Kauli kama hizi zimejengwa katika akili za wengi, kutokana na mafundisho ya viongozi wa dini za Kikristo duniani, zinazofundisha kwamba mtu akifa anakwenda mahali fulani. (Mbinguni).
ReplyDeleteKwa sisi tunaoiamini Biblia, inasema hivi: Wafu hawajui neno lolote...... Mhubiri 9:5-10.
Mtu anapokufa anarudi mavumbini. (Mwanzo 3:19 ;Mhubiri 3:20 ; Mwanzo 47:30 ; Zaburi 88:10 ; Zaburi 115:17 ; Zaburi 146:4 ; Isaya 38:18 ; Yohana 11:11.) Kwa sababu wote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, ndio maana tunakufa Warumi 5:12.Wanasubiri ufufuo utakaofanywa kupitia Mfalme Yesu kristo (Yohana 5:28,29)Maneno kama "Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana na libarikiwe" yamenukuliwa kutoka kwa Ayubu (Mhubiri1:21) Ayubu aliyatamka maneno hayo AKIDHANI kwamba ni Mungu aliyesababisha mateso yake. Kumbe ni Shetani Ayubu 1:6-20. Hivyo hivyo leo, mengi machungu yanapotupata "tunamsingizia Mungu" kwamba ni mapenzi yake. Kwa mfano, mtu anakunywa pombe kupita kiasi, anaendesha gari, anagonga mti, anakufa. Utasikia maneno kama:- "Kama aliandikiwa kufa kwa aksidenti lazima afe tu!", "Mungu amempenda zaidi", "Mungu amechukua kiumbe chake", "Mungu amechuma ua lake", n.k.Hembu tutafakari. Mungu amezuia ulevi, kwa hiyo kama asingekuwa mlevi kwa kutii aizo hilo, angeendesha kwa uzembe agonge mti?..... Na je, Mungu anajisikiaje anapotajwa kuwa ndiye msababishi wa kifo hicho?.... Kama ungekuwa wewe, ungejisikiaje?
Ndio maana katika sala ya Bwana ya kielelezo, tunasali Jina la Mungu litukuzwe (litakaswe),(Mathayo6:9,10) maana limelundikiwa lawama nyiiingi isivyo haki.