Nafasi Ya Matangazo

March 03, 2012

Ng'ombe wa Masiki hazai na akizaa huzaa dume tena linakuwa maksai...usemi huu ndio ulioikuta timu ya soka ya Yanga katika mchezo wao wa marudiano hii leo huko Misri dhidi ya Zamaleki. 

Yanga iliyoshusha kikosi kamili dimba la Chuo cha Kijeshi cha Miri iliambulia kichapo hicho na kufanya timu hiyo kwenda nje ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya magoli 2-1 kufuatia mchezo wa awali kutoka sare ya goli 1-1 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka Misri zinasema kuwa Yanga huenda ingechapa goli 2 lakini Zamaleki ilikosa penati baada ya mchezaji wake mmoja kuchezewa ndivyo sivyo na Chuji ambaye alilambwa kadi nyekendu. 

Posted by MROKI On Saturday, March 03, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Acha wakome wana mdomo sana na kufungwa kwao kumepunguza midomo.

    Haya mashindano ya kimataifa Yanga hawawezi wamwachie MNYAMA wao waendelee kunyanyasa timu za humu ndani tu.

    Walidhani Zamalek ni sawa na MTIBWA wanayofunga tatu.

    ACHA WAKOME NA MIDOMO YAO WANADHANI MPIRA UNACHEZWA MDOMONI? ha ha ha ha haa YANGAAAAAA SAFI MKOME

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo