Timu ya Soka ya Uganda leo imetandika timu ya Tifa ya Tanzania Bara The Kilimanjaro Stars kwa magoli 3-1 katika mchezo qwa pili wa Nusu fainali ya michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja kabla ya Tanzania bara kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Kwa matokeo hayo Kili Stars leo ndio watakuwa wamelikabidhi rasmi kombe hilo kwa timu za Uganda na Rwanda kwani ndio alikuwa Bingwa mtetezi, kuliwania kwani ndio timu zilizofuzu kucheza fainali. Sasa Kili Stars itaungana na Sudan katika kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.





0 comments:
Post a Comment