Nafasi Ya Matangazo

December 09, 2011

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 8 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck sadick, akizungumza jukwaani kutoa salam za sherehe hizo kwa wananchi.
  Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo
  Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Koba, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria Mkesha wa Sherehe za Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru. 
Vijana wakishangia burudani iliyokuwa ikitolewa jukwaani na makundi mbalimbali ya sanaa, wakati wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo .
Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.
Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba kupitia Chama cha Wananchi CUF, Hamad Rashid, akijumuika na vijana wa CCM pamoja na Msindai kucheza miondoko ya Taarab, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo
 Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakiimba jukwaani ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani maalum ya kusherehekea sherehi hizo.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Kapten John Komba, akiongoza kundi lake la Kwaya kuimba wimbo maalum wa Maadhimisho ya Sherehe hizo jukwaani.
Baadhi ya Wabunge na wananchi wakimtunza Kaptein John Komba wakati akiimba jukwaani.
Mbunge John Shibuda, akipagawishwa na ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo, iliyokuwa ikipigwa na wasanii wa kundi  la JKT Mgulani. 
Posted by MROKI On Friday, December 09, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo