Nafasi Ya Matangazo

December 19, 2011

Baba Askofu Mkuu Nestory Timanywa wa Jimbo la Bukoba kanisa Katoliki katika Mgeni rasmi Dk Emmanuel Nchimbi Waziri wa habari Vijana Utamaduni na Michezo kulia na Paroko wa Parokia ya Kasambya Padri Christopher Mwoleka, wakikata keki katika ibada maalum ya Jubilee ya miaka 75 ya Parokia ya Kasambya Kyaka Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera jana. 
 
Katiba ibada hiyo ambayo mahubiri yalitolewa na Askofu msaidizi wa Jimbo la Methodius Kilaini, akihubiria waumini wa Parokia hiyo pamoja na wageni mbalimbali waliofika katika jubilee hiyo ya miaka 75 ya kanisa hilo Parokia ya Kasambya, alisema wanamshukuru mungu kwa kuwafikisha hapo mpaka kusherehekea jubilee hiyo. 
 
Lakini akasema makovu ya vita vya Kagera alivyanzisha Nduli Idd Amini hayawezi kusahaulika kwa wakatoliki wa Kasambya na wanakagera wote, kwani kanisa hilo lilipata athari kubwa kutokana na vita hivyo, ambapo mpaka sasa bado uchumi wa watu wengi haujatengamaa. 
 
Lakini pia aliwashukuru vijana wao wote waliozaliwa Kasambya huko Kyaka Wilaya ya Misenyi na kusema, wamekuwa na moyo mzuri kwa kasaidia maendeleo ya kanisa hasa Parokia yao ya Kasambya, huku akiwataja baadhi wakiongozwa na Dionis Malinzi ambaye jana aliendesha harambee ya kujenga nyumba ya kuishi Mapadre na maaskofu, na kufanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni 10 huku Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi. akiahidi kutoa mabati ya kukamilisha nyumba nzima. 
Picha zaidi ingia Fullshangwe Blog. 
Posted by MROKI On Monday, December 19, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo