Nafasi Ya Matangazo

December 19, 2011

Zanzibar, Jumatatu Disemba 19, 2011: Zantel, kampuni ya mawasiliano inayoongoza Zanzibar inafuraha ya kutangazia umma uteuzi wa Bw. Mohammed Mussa kuwa Mkuu wa Kibiashara Zanzibar kuanzia Jumanne Disemba 13, 2011.

Nafasi hii mpya ni mojawapo ya mikakati ya Zantel kuboresha shughuli zake za kibiashara Zanzibar.
Mohammed Mussa atakuwa anasimamia shughuli zote za kibiashara Zanzibar na atawajibika kwenye masuala ya masoko, mauzo kitengo cha makampuni pamoja na wateja wa malipo ya kabla na huduma kwa wateja.

Ahmed Mokhles, Afisa Mkuu wa Kibiashara Zantel akizungumzia uteuzi wa Bw. Mohammed Mussa alisema uteuzi wake ni kimkakati kuupa umuhimu kazi za kibiashara pamoja na wateja wetu wa Zanzibar.

“Zantel tunaongoza soko la Zanzibar kimawasiliano Na Kama Mkuu wa Kibiashara wa Zanzibar jukumu lake Ni kuhakikisha tunaendelea kuongoza pamoja Na kutekeleza ahadi tulizozitoa Kwa wateja wetu Kwa njia ya haraka, kuaminika na uzoefu wa utoaji wa huduma kwa wateja.” Alisema Bw. Mokhles.

Bw. Mussa alijiunga na kampuni ya Zantel miaka 12 iliyopita na kuanza kazi kwenye idara ya teknologia ya mawasiliano na kushika nyadhifa mbalimbali kwenye idara hiyo. na kabla ya uteuzi huu alikuwa anashikilia cheo cha Meneja Mwandamizi wa Mauzo kitengo cha makampuni.
Posted by MROKI On Monday, December 19, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo