Sheikh Khamis Haji Khamis |
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi katika nyadhifa mbalimbali, ambapo amemteua Sheikh Saleh Omar Kabhi kuwa Mufti wa Zanzibar.
Dk. Shein pia, amemteua Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Wengine ni Bwana Muumin Khamis Kombo ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashataka, Zanzibar. Bwana Abdulrahman Mwinyi Jumbe Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Dk Shein pia, amemteua Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa kuwa Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji, Bwana Burhan Saadat Haji kuwa Mshauri wa Rais Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ambapo Bwana Issa Ahmed Othman ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Utalii.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee, uteuzi huo umeanza jana tarehe 25 Septemba.
0 comments:
Post a Comment