Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa
Utekelezaji wa Mpango wa Ufadhili wa Kuunganisha Umeme kwa Wananchi kati ya
TANESCO na CRDB, hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 02 Oktoba 2026.
(kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Dkt. Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkurugenzi
wa TANESCO Razaro Twange)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa na Viongozi mbalimbali wakishiriki hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Tarehe 02 Oktoba 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma
Homera pamoja na Viongozi mbalimbali, akizindua Mpango wa Ufadhili wa
Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Tarehe 02 Oktoba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akihutubia wakati wa hafla ya utiaji Saini
Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi,
kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar
es Salaam. Tarehe 02 Oktoba 2026.

Viongozi, wadau na wananchi mbalimbali
wakishiriki katika hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa
Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi.
Tarehe 02 Oktoba 2026.
Viongozi, wadau na wananchi mbalimbali
wakishiriki katika hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa
Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi.
Tarehe 02 Oktoba 2026.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wito
kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na wadau husika wa
sekta binafsi kuandaa mpango utakaowawezesha wananchi kununua umeme kwa mkopo
kama ilivyo mikopo katika mitandao ya simu ili kuwasaidia wananchi wanapokuwa
na uhitaji wa umeme lakini hawana fedha.
Makamu
wa Rais ametoa wito huo wakati wa hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa
Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema hatua hiyo
itaweza kusaidia wananchi kuendelea kutumia huduma ya umeme na kufanya
uzalishaji mali au mahitaji ya nyumbani hata pale wanapokuwa na changamoto ya
fedha ya kununua umeme huo.
Aidha,
Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kuendeleza mradi ulioanzishwa chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha wananchi wanaoishi
mazingira yanayofanana na kijijini lakini mipaka ya kiutawala inamtambua yupo
mjini wanaunganishiwa huduma ya umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama ya
wananchi wa vijijini. Amesema yapo maeneo ambayo ni mipaka ya kiutawala
inawatenganisha wananchi kati ya mijini na vijijini lakini wananchi hao maisha
yao yanafanana.
Makamu
wa Rais, amesema azma hiyo, inalenga kufikia lengo la kitaifa, malengo ya “mission
300” pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, kuhakikisha huduma ya umeme
inamfikia mtanzania kwa gharama nafuu.
Makamu
wa Rais ameipongeza TANESCO na Benki ya CRDB kwa hatua hiyo muhimu inayolenga
kuimarisha na kuboresha maisha ya wananchi kwa kupata huduma ya umeme. Amesema ushirikiano huo ni mfano bora wa
namna ya Taasisi za Umma na Sekta Binafsi zinavyoweza kuwaunganisha watanzania
na kuwekeza nguvu na rasilimali ili kutatua changamoto zinazowagusa wananchi
moja kwa moja.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Abdulmajid Nsekela amempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
maono na uwepo wa Dira ya Maendeleo 2050. Amesema Serikali na Sekta binafsi
kupitia ubunifu itawezesha kutekelezwa na kufanikiwa kwa Dira 2050 inayolenga
kujenga uchumi mkubwa, yenye kuzalisha ajira, wenye ushindaji, unaotumia
teknolojia na kuboresha maendeleo ya wananchi.
Amesema
Benki ya CRDB imedhamiria kuwa mshirika wa maendeleo yan chi kwa kutumia uwezo
wa kifedha, teknolojia iliyopo, rasilimali ya wataalamu waliopo, mtandao uliopo
na ubunifu katika kusaidia kutatua changamoto ya maendeleo ya Taifa.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANESCO, Razaro Twange amesema upatikaji wa umeme umeendelea kuongezeka
nchini na ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme na kusambaza umeme
ikiendelea kujengwa. Amesema Tanzania inafikia megawati 4500-4600 hivi sasa
huku kukiwa na mtandao wa kiliometa 9000 za kusafirisha umeme, na mtandao wa
zaidi ya kilometa 220,000 wa njia za kusambaza umeme.
Utiaji
wa Saini wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya
Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), utawezesha wananchi wa
maeneo ya vijiji kuunganishwa bure huduma ya umeme kutokana na ruzuku kutoka
Benki ya CRDB, na kwa wananchi maeneo ya mijini watapewa huduma hiyo kwa mkopo
wa riba nafuu ambao wataweza kuunganishwa umeme na kufanya shughuli za
uzalishaji mali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa Viongozi mbalimbali katika picha ya
pamoja na Viongozi wa mitaa na vijiji mara baada ya hafla ya utiaji Saini
Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi,
kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar
es Salaam. Tarehe 02 Oktoba 2026.












0 comments:
Post a Comment