Nafasi Ya Matangazo

September 26, 2011

“Anybody can dig a hole and plant a tree. But make sure it survives. You have to nurture it, you have to water it, you have to keep at it until it becomes rooted so it can take care of itself. There are so many enemies of trees.”

Kifo hakina huruma walahakichagui masikini wala tajiri, Msomi au Mbumbumbu, Mkulima au mfanyakazi na hakichagui mtoto au mtu mzima, saa ikifika na ukaitwa utaitika hata uhangaike kwa namna gani. 

Mshindi waTuzo ya Nobel 2004 Nobel Prof. Wangari Maathai ameitwa akaitika hatunae tena duniani, jina la Bwana lihimidiwe.

Wangari (71)amefariki usiku wakumkia leo katika Hospitali Kuu ya Nairobi alipolazwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani .

Wangari alizaliwa Aprili 1, 1940  katika Kijiji cha Ihithe, Tarafa ya Tetu, Wilayani Nyeri.

Wangari ambaye ni miongoni mwawanawake mashuhuri nchini Kenya aliyetokea kukubalika na jamii, kupendwa na kuheshimika duniani kote na mwanake ambaye wakenya walikuwa wakijivunia baada ya kutangzwa kuwa mshindi watuzo ya Nobelupande wa Mazingira kutokana na mchango wake mkubwa katika uhifadhi mazingira.

Wangari atakumbukwa sana na Wakenya pale alipo pambana vilivyo na Rais Moi,  kutetea kujengwa kwa mnara katika eneo la viwanja vya Uhuru Park.

Pia Wangari atakumbukwa vile alivyo shiriki katika mgomo wasiku kadhaa wakutokula pamoja na wanaharakati wqengine nchini Kenya wakushinikiza wafungwawa kisiasa nchini humo waachiliwe huru.

Mwanamazingira huyo pia atakumbukwa alipo pambana tena vilivyo na utawala wa Rais Moi juu ya kugawa msitu wa Karura kwa maswahiba zake.

Hizo ni miongoni tu wa juhudi zake alivyo pambana kwa hali na mali kuhakikisha bustani ya Uhuru Park ambayo hii leo Wakenya wengi wanaitumia katika kupunga upepo mwishoni mwa wiki na familia zao ama wapitanjia wanaoamua kupumzika hapo baada ya pilika pilika za kutwanzima na misitu ya Kenya inabaki bila kuguswa.

Rest in Peace, Mama. You were one of a kind.
Posted by MROKI On Monday, September 26, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo