Wanafunzi wa Shule ya Msingi Donbosco Dar es Salaam wakicheza ngoma ya Mganda wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo. Anaewaongoza ni mtoto Mecky Tegete aliyekuwa kivutio kwa wengi.
Wanafunzi wakifuatilia sherehe hizo...
Ilifika wakati wa kucheza na kufurahi...watoto wa St. Kayumba walijimwaga kisawasawa na vibwebwe kiunoni wakicheza Alaji.
watoto kutoka "ST Mroki" wao mambo ya alaji yaliwapitia kushoto na Alaji wao iliwashinda wakasimama wima.
Hakika mtoto wa Afrika anahitaji sana Ulinzi, kupendwa, kupata huduma safi na bora, elimu, na kila hali ambayo itamfanya mtoto wa Afrika hasa Tanzania akue vyema katika malezi yaliyojaa maadili ili kuepusha kuwapo kwa watoto wa mtaani ambao chanzo chake ni malezi mabaya katika familia zetu.
TUPAMBANE NA ONGEZEKO LA WATOTO WANAOISHI MTAANI.
0 comments:
Post a Comment